23.3 C
Dar es Salaam
Thursday, June 13, 2024

Contact us: [email protected]

Klopp awatumia salamu Man City

LIVERPOOL, ENGLAND 

KOCHA wa timu ya Liverpool, Jurgen Klopp, ametuma salamu kwa mabingwa wa Ligi Kuu England, Manchester City huku akiwaambia msimu ujao wa ligi watakuwa wanafungika kwa urahisi.

Msimu mpya wa Ligi Kuu England, unatarajiwa kufunguliwa mwishoni mwa wiki ijayo, hivyo kocha huyo anaamini safari hii hatokuwa kama msimu uliopita kuangalia matokeo ya mchezo wa mwisho ili kutangazwa bingwa.

Mbali na Liverpool kushika nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi msimu uliopita, lakini waliweza kutwaa ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Katika maandalizi ya msimu mpya wa Ligi, Liverpool hawajaonesha ubora wao na kuwapa wasiwasi mashabiki. Katika michezo sita ya kujipima nguvu wamefanikiwa kushinda michezo miwili na michezo hiyo waliyoshinda ni dhidi ya timu za madaraja ya chini kama vile Tranmere Rovers na Bradford City.

Lakini walikubali kichapo kutoka kwa Borussia Dortmund, Sevilla Napoli huku wakitoa sare dhidi ya Sporting CP. Hata hivyo kocha huyo amedai wanatakiwa wapambane kwa kiasi kikubwa ili kuhakikisha wanafanya vizuri msimu ujao.

“Bila shaka, ninaamini msimu ujao hautokuwa kama uliopita kwa Farasi wawili kukimbizana hadi hatua ya mwisho, kuna timu nyingi zenye wachezaji wazuri msimu ujao, tunajua Man City wanapewa nafasi kubwa ya kufanya vizuri, lakini timu zingine zinapambana kwa ajili ya kuifunga timu hiyo na sisi ni miongoni mwa timu hizo ambazo zinawania kuifunga City. Tunaimani tutafanya vizuri bila kujali michezo ya kirafiki kabla ya kuanza kwa ligi tunafanyaje,” alisema kocha huyo.

Hata hivyo, kocha huyo aliongeza kwa kummwagia sifa mchezaji wake mpya Harvey Elliott ambaye juzi alicheza mchezo wake wa kwanza baada ya kusajiliwa ikiwa ni siku hiyo ambaye amejiunga akitokea Fulham.

“Ndio maana tumemsajili, ameonesha kiwango cha hali ya juu na ninaamini atazidi kufanya hivyo hapo baadae baada ya kuzoea mazingira,” aliongeza.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles