26.8 C
Dar es Salaam
Saturday, September 7, 2024

Contact us: [email protected]

Ozil, Kolasinac akili zao hazijakaa sawa

LONDON, ENGLAND 

KOCHA wa timu ya Arsenal, Unai Emery, ameweka wazi sababu ya kuwaacha nje nyota wao Mesut Ozil na Sead Kolasinac katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Lyon ni kutokana na kutokuwa sawa kiakili.

Mapema wiki iliopita wachezaji hao walivamiwa na majambazi jijini London na kunusurika kuchomwa kisu katika shambulio la kujaribu kuiba gari.

Wachezaji hao walivamiwa wakiwa wanatoka mazoezini, lakini hawakuumizwa dhidi ya majambazo hao wawili ambao waliopambana na Kolasinac.

Emery amedai mbali na wachezaji hao kutoumizwa kwenye tukio hilo, lakini bado akili zao hazijakaa sawa kwa asilimia 100 na ndio maana akawaacha nje kwenye mchezo huo ambao Arsenal walikubali kichapo cha mabao 2-1.

“Kila mchezaji ana umuhimu wake ndani ya kikosi na kila tukio kwa mchezaji linaweza kuwa na maana tofauti kwa kipindi hicho, hivyo tuliamua kuwaacha wachezaji hao nje ya uwanja kutokana akili zao hazikuwa sawa.

“Walikuwa wanatakiwa kupumzika na familia zao kwa muda ili warudi katika hali ya kawaida kwa ajili ya kuitumikia timu. Kikubwa kitu ambacho tunakitaka ni kuwaona wachezaji hao wakiwa na amani, wakijiona wapo sehemu salama,” alisema kocha huyo.

Hata hivyo polisi jijini London, wameweka wazi kwamba, bado wanaendelea na uchunguzi juu ya tukio hilo kwa kuwatafuta watuhumiwa.

Baada ya tukio hilo, wachezaji hao walitumia kurasa zao za mitandao ya kijamii na kuposti video ambayo ilikuwa inaonesha tukio zima la uvamizi huo na tukio hilo lilirekodiwa na camera za CCTV.

Emery anaamini wataanza vizuri kwenye mchezo wao wa ufunguzi wa Ligi Kuu dhidi ya Newcastle ambapo The Gunners watakuwa ugenini Agosti 11. 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles