MKAZI wa Mwananyamala, Ahmed Mudhihiri (26), amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Wilaya Kinondoni, Â Â Dar es salaam akikabiliwa na mashtaka matatu yakiwamo ya ubakaji na kufanya udanganyifu kuwa yeye ni mtoto wa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).
Akisomewa mashtaka yake mbele ya Hakimu Caroline Kiliwa, Mwendesha Mashtaka, Neema Moshi, alidai Julai 6  katika eneo la Hoteli ya White Sands  Mbezi Africana   Dar es Salaam, mshitakiwa alimbaka binti (jina limehifadhiwa).
Shitaka la pili ni kuwa  kati ya Juni 17 na Julai 7 mwaka huu   Dar es Salaam, alidanganya kuwa yeye ni Mwamvita Makamba.
Katika shitaka la tatu, mshitakiwa alidaiwa kati ya Juni 18 na Julai 7 mwaka huu, Dar es Salaam, alijitambulisha kuwa yeye ni Edd mtoto wa   CAG.
Wakati huohuo, mkazi wa Msasani, Francis Benjamin (45), amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Wilaya Kinondoni, Â Â Dar es Salaam kwa shitaka la ulawiti.
Mwendesha Mashtaka Ramadhan Mkimbu, alidai mbele ya Hakimu Frank Moshi, kuwa kati ya Aprili 19 na Aprili 24 mwaka huu alimlawiti kijana mwenye umri wa miaka 12.
Mshtakiwa alikana kutenda shitaka hilo na  kesi iliahirishwa hadi Oktoba 2 mwaka huu.