24.4 C
Dar es Salaam
Thursday, October 31, 2024

Contact us: [email protected]

Kizimbani kwa kuiba hospitali

ERICK MUGISHA-DAR ES SALAAM

WATU wane wamepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni, Dar es Salaam kwa makosa manne ikiwemo wizi.

Waliofikishwa mahakamani ni Erick Marcus (20) mkazi wa Kiwalani, Baraka Samora (20) mkazi wa Ubungo Kibo, David Hakimu (32) mkazi wa Ubungo Makoka na Abdallah Issah (36) mkazi wa Ubungo Kibo.

Mwendesha Mashtaka wa Serikali, Yussuf Aboud, akiwasomea mashtaka mbele ya Hakimu Frank Mushi, alidai mashtaka matatu yanawakabili Erick Marcus na Baraka Samora ambao tarehe isiyo fahamika wanadaiwa walipanga njama ya kuvunja na kuiba katika jengo la Hospitali ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).

Katika shitaka la pili, Mei 26,  maeneo ya Hospitali ya  Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Wilaya ya Ubungo, wanadaiwa walivunja na kuingia kwenye hospitali ya chuo.

Katika shitaka la tatu, Mei 26, maeneo ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaamm Wilaya ya Ubungo wanadaiwa waliiba  TV tatu za nchi 32 aina ya Sony zenye thamani ya Sh 2,383,785/- mali ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Katika shitaka la nne, linawakabili David Hakimu na Abdallah Issah ambao wanadaiwa Juni 18, 2019 maeneo ya Ubungo Wilaya ya Ubungo Dar es Salaam, walipatikana na mali ya wizi ambazo ni TV tatu nchi 32 aina ya Sony zenye thamani ya Sh 2,383,785/-.

Washtakiwa wote wanne walikana kutenda makosa hayo na hakimu Mushi alisema dhamana ipo wazi kwa masharti ya kuwa na wadhamini wawili kwa kila mmoja, mwenye barua za utambulisho kutoka Serikali za mtaa na wenye kusaini bondi ya sh 1,000,000.

Washtakiwa wote walishindwa kutimiza masharti ya dhamana na kurudishwa rumande hadi kesi yao itakapokuja kusomwa tena Agosti 1, 2019.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles