China
Kasi ya uzazi wa watoto nchini China, imeshuka zaidi kufikia kiwango cha chini kabisa tangu taifa hilo lilipoanzishwa mwaka 1949. Licha ya juhudi za kuwahamasisha wanandoa kuzaa watoto Zaidi.
Mwaka 2016 China ilifuta sera yake ya mtoto mmoja kwa kila familia na kuwaruhusu wanandoa kuzaa watoto wawili.
Lakini sera hiyo inaonekana haikusaidia katika ongezeko la idadi ya watu huku gharama za maisha zikipanda miongoni mwa wanandoa wanaozingatia kupata mtoto.
Kiwango cha uzazi mwaka 2018, kilishuka kuliko mwaka uliotangulia wa 2017. China ina jumla ya watu karibu bilioni 1.4.