Na Averine Kitomary, Mwanza
Kaimu Mkuu wa Mabaara ya Mamlaka ya Dawa, Vifaa Tiba na Vitendanishi(TMDA) Kanda ya Ziwa, Bugusu Nyamweru amesema utumiaji wa vitakasa mikono ‘Sanitizer’ visivyo na ubora unaweza kuwa na madhara makubwa ikiwemo kuwaka moto, kuharibu ngozi na kuwashwa.
Nyamweru amewaambia Waandishi wa Habari waliotembelea Maabara hiyo jijini Mwanza.
Amesema ni muhimu kiwango cha kilevi(alcohol) kiwe ni kile kinachohitajika ambacho hakitakiwi kupungua wala kuongezeka.
“Kama utatumia sanitaizer inakiwango kidogo cha alcohol wadudu wanatakiwa kufa hawatapata madhara hiyo ni hasara kwa sababu lengo halijafikiwa.
“Endapo kiwango cha alcohl kimezi pia mdhara ni makubwa zaidi kuna uwezaka na mtumiaji kuwaka moto, kuwashwa au kupata madhara katika ngozi hivyo watengenezaji wanatakiwa kuwa makini,”amefafanua Nyamweru.
Amesema maabara hiyo inamashine ya kisasa ambayo inauwezo mkubwa wa kupima vipukusi ikiwemo vitakasa mikono inayoitwa Sanitezer machine.
“Tuna mashine ambayo inahusika katika uchunguzi wa vitakasa mikono hii ni moja wapo ya vipukusi ambayo ipo katika kundi ya kuua vimelea vya bakteria au vimelea vinavyosababishwa na virusi.
“Mashine hii inatumika kuangali ubora wa alcohl iliyoko ndani ya vitakasa mikono ni mashine ndogo lakini inafanya kazi kwa kutumia mvuke kuondoa kiwango cha pombe na pia kinakusanywa katika kifaa,”ameeleza.
Amesema baada ya mvuke kutolewa kiwango cha kilevi(alcohol) hupimwa kwa kutumia kifaa kinachoitwa hyrometer.
“Kifaa kingine kinaitwa (Steam Distiller) hii inachuja formula iliyoko ndani ya vitakasa mikono had sasa tumeweza kupima sampuli zaidi ya 90 ya vitakasa mikono na ufanisi wake ni mzuri.
“Viwango (Standarnd) vinavyotumika katika upimaji tunaangalia kama ni asilimia 70 tunaangalia isifike mfano vitakasa mkono haitakiwa kuwa chini asilimia 60 kwahiyo tutatengeneza kiwango kinachofahamika kisha tutapima kwa utaratibu huohuo na tutalinganisha na sampuli yetu ambayo pia tutaipima kwahiyo majibu yatakayopatikana hapo tutajiridhisha kwamba kweli sampuli yetu inakiwango inachotakiwa kwa kulinganisha kwa kiwango cha kimataifa,”amefafanua Nyamweru.
Amesema kuwa mashine hiyo inauwezo wa kufanya kazi kwa muda wa dakika nne hadi sita.