26.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, May 22, 2024

Contact us: [email protected]

Kiwanda hatari chagundulika Dar

Hiiti SilloNa Jonas Mushi, Dar es Salaam

MAMLAKA ya Chakula na Dawa (TFDA) imebaini kuwapo kiwanda hatari cha manukato (perfume) feki Dar es Salaam.

Manukato yanayotengenezwa na kiwanda hicho yanaitwa Same.

Mamlaka pia imekamata shehena ya manukato ya thamani ya Sh milioni 107.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Mkurugenzi Mkuu wa TFDA, Hiiti Sillo, alisema shehena hiyo ilikamatwa Februari 23, mwaka huu.

Sillo alisema shehena hiyo ilikamatwa katika duka la Dk. Mohamed Gwao lililopo Sinza kwa Remmy, Manispaa ya Kinondoni.

“Baada ya kukamatwa shehena hiyo, mmiliki wa duka hilo alihojiwa na kusema kuwa aliagiza bidhaa hizo kutoka Uturuki, Desemba 27, mwaka jana,” alisema.

Sillo alisema uchunguzi uliendelea kwa kushirikiana na polisi na Februari 29, mwaka huu ndipo kilipogundulika kiwanda kinachotengeneza bidhaa hizo katika eneo la Tuangoma, Mtaa wa Goroka, Manispaa ya Temeke.

“Februari 23, mwaka huu tulipata taarifa ya kuwapo duka lenye ‘perfume’ feki maeneo ya Sinza kwa Remmy. Tulipofuatilia tulikamata shehena ya chupa 5,350 zenye thamani ya Sh milioni 107,” alisema Sillo na kuongeza:

“Baada ya tukio hilo tuliendelea na uchunguzi na jana (juzi) TFDA Kanda ya Mashariki ilifanya upekuzi katika nyumba iliyotajwa kuwa ni ya Mwanaidi na kubaini kuwapo kiwanda kinachozalisha ‘perfume’ ya Same.”

Sillo alisema katika nyumba hiyo vilikamatwa vifaa vya maabara na malighafi zikiwamo kemikali zinazotumika kutengeneza manukato hayo.

Pia zilikamatwa lebo zinazobandikwa kwenye manukato hayo ambazo zinaonyesha kuwa yanatengenezewa Uturuki na yanaingizwa nchini kutokea Ufaransa.

Alisema alikamatwa mwangalizi wa nyumba hiyo, Fatuma Selemani, ambaye anashikiliwa na polisi ili kusaidia upelelezi na jalada la polisi limefunguliwa katika Kituo cha Polisi Wilaya ya Kipolisi Mbagala.

Sillo aliwataka wananchi walionunua manukato ya Same waache kuyatumia na badala yake wayapeleke katika ofisi za TFDA au katika vituo vya polisi vilivyopo karibu yao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles