23 C
Dar es Salaam
Wednesday, September 18, 2024

Contact us: [email protected]

Kivumbi cha CCM Majimbo matano leo

Patricia Kimelemeta na Esther Mnyika

UPIGAJI wa kura za maoni zinazorudiwa katika majimbo matano leo nchini katika Chama Cha Mapinduzi (CCM)unatarajiwa kuwa na mvutano mkubwa.

Majimbo yanayorudia uchaguzi na mikoa yake kwenye mabano ni Busega (Simiyu), Kilolo (Iringa), Rufiji (Pwani), Makete(Njombe)na Ukonga(Dar es Salaam).

Kamati Kuu ya CCM iliamuru uchaguzi huo urudiwe baada ya kubaini rafu na ukiukwaji wa taratibu za uchaguzi wakati wa kura za maoni ambapo pia matokeo yake yanapaswa kuwasilishwa haraka katika ngazi za juu kwa ajili ya uamuzi wa mwisho.

Kwa upande wake, kura za maoni katika Jimbo la Ukonga Mjini Dar es Salaam unatarajiwa kuanza saa tatu asubuhi leo.

Akizungumza na gazeti hili jana, Katibu wa CCM Wilaya ya Ilala, Ernest Charles alisema kuwa, kamati ya siasa ya wilaya hiyo iliitisha kikao chake jana kwa ajili ya kupanga ratiba ya kurudiwa kwa uchaguzi huo.

“Baada ya kupewa taarifa kutoka ngazi za juu, kamati ya siasa ya wilaya ilikutana kwa ajili ya kujadili na kupanga ratiba ya kurudiwa kwa uchaguzi huo kama tulivyoambiwa na kamati kuu,”alisema Charles.

Aliongeza kutokana na hali hiyo, wanachama wa chama hicho watarudia kupiga kura za maoni ili kumchangua mwanachama atakayepeperusha bendera ya CCM katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu.

Charles aliwataka wanachama wa chama hicho kujitokeza kwenye vituo vya kupigia kura ili waweze kutumia haki yao ya msingi ya katiba ya chama.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles