26.1 C
Dar es Salaam
Friday, January 3, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Kitimutimu cha Makonda na mawaziri

Na AGATHA CHARLES – Dar es Salaam


KAMPENI ambazo amekuwa akizibuni au kuzianzisha Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ndani ya miaka mitatu ya utawala wa Rais Dk. John Magufuli, zinaonekana kuwatoa jasho baadhi ya mawaziri.

Uchunguzi na taarifa mbalimbali zilizokusanywa na MTANZANIA Jumapili katika kipindi hicho, unaonesha kampeni iliyozua mjadala wa sasa wa sakata la mashoga, iliyoanzishwa na Makonda si ya kwanza kuwaibua na hata kuwalazimisha mawaziri ama kutoa ufafanuzi, kuboresha au kuzipinga.

Kampeni yake ya sasa ya kutokomeza vitendo vya ushoga akiwataka wakazi wa mkoa wake kumtumia majina ya watu wanaojihusisha na vitendo hivyo, ilionekana wazi kutikisa ndani na nje ya mipaka ya Tanzania kiasi cha kuzilazimu wizara mbili kuitolea ufafanuzi.

Wizara hizo ni Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na ile ya Mambo ya Ndani ya nchi.

Kabla wizara hizo hazijatoa matamko yake, aliyekoleza mjadala wa sakata hilo alikuwa ni Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamis Kigwangalla ambaye kupitia ukurasa wake wa Twitter aliandika ujumbe; “Machoko hawatoingia hapa, wataishia airport na kurudishwa walikotoka”, akionekana kuunga mkono kampeni hiyo ya Makonda.

Andiko hilo la Kigwangalla ambalo halikudumu muda mrefu baada ya kulifuta, lilionekana kuwakera wadau mbalimbali na hasa mawakala wa kuleta watalii kutoka nje ya nchi ambao walitafsiri kampeni hiyo kama uvunjifu wa haki za binadamu na hata kutishia biashara ya utalii.

Kwa habari zaidi jipatie nakala yako yab gazeti la MTANZANIA.
- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles