26.1 C
Dar es Salaam
Friday, January 3, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Kisima cha gesi Mtwara hatarini kumezwa na bahari

FLORENCE SANAWA, MTWARA

WAZIRI wa Nishati, Medard Kalemani amesema kisima cha gesi asilia kilichopo Mnazi bay, Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara, kiko hatarini kumezwa na mmonyoko wa ardhi unaosababishwa na bahari.

Kisima hicho ambacho kiko mita chache kutoka baharini, kimekumbwa na matukio mbalimbali ya kuhatarisha usalama wa eneo hilo ambako mwaka 2015 zaidi ya mita 150 za ardhi zilimezwa na bahari na kusababisha eneo hilo kuwa katika hatari zaidi kwa mitambo iliyopo.

Akizungumza baada ya kutembelea kisma hicho, alisema endapo uzalishaji utasimama hali ya umeme na matumizi ya gesi asilia yanaweza kusimama.

Waziri alizitaka taasisi husika kulichukulia jambo hilo kama dharura kupata ufumbuzi wa haraka.

Kalemani alisema jitihada za makusudi zinapaswa kuchuliwa kunusuru eneo hilo ambalo ni muhimu kwa uchumi wa nchi ikizingatiwa hivi sasa vipo viwanda na familia ambazo zinatumia gesi majumbani huku mikoa ya Lindi na Mtwara ikipata huduma hiyo kupitia uzalishaji wa umeme.

Alisema kutokana na udharura huo maandalizi yaanze mapema kwa sababu watakaporuhusu kufanyika uchunguzi (study) zinaweza kuchukua muda mrefu zaidi hali ambayo inakifanya kiwanda hicho kuwa katika hatari zaidi kiwa usalama hivyo jambo hilo lifanyike kwa dharura baada ya kupata suluhisho la dharura.

“Unajua gesi kwa sasa ina matumizi makubwa na inahitajika zaidi, endapo mmomonyoko huo ukiendelea utaathiri sehemu kubwa ya maeneo ambayo hutumia gesi kwa ajili ya umeme na matumizi ya viwandani.

“Wakati wowote hiki kisima kitaingia hatarini, ni jambo la dharura, tusikubali litukumbe ndiyo hatua zichukuliwe, fikiri haya maji yafikie hapa, mnaweza kukosa hata sehemu ya kupita, mnafanya utafiti gani wakati mnaona maji yanafi ka?” alisema.

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Maurel & Prom, Elias Kilembo, alisema eneo hilo limekuwa katika hatari zaidi baada ya mmomonyoko wa ardhi kujitokeza katika eneo hilo.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles