27.5 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 30, 2021

Serikali yaiangukia Benki ya Ulaya

NA AZIZA  MASOUD-DAR ES SALAAM

SERIKALI  imeiomba Benki ya Mendeleo Ulaya (EIB) kuharakisha mchakato wa utoaji kibali  cha kupata mkopo wa fedha za kujenga viwanja vinne vya ndege vyenye hadhi ya kimataifa ili kuinua sekta ya miundombinu nchini.

Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe, alipokuwa akifungua mkutano wa 12 wa kupima utendaji wa sekta ya uchukuzi nchini.

Alisema miezi 24 sasa imepita tangu waliposaini mkataba huo wa kupatiwa kibali cha kupata fedha hizo na benki hiyo.

Mhandisi Kamwelwe alisema ucheleweshwaji huo unatokana na benki hiyo kuhoji uwezo wa Wakala wa Barabara nchini (Tanroads) kuweza kusimamia ujenzi wa viwanja hivyo nchini.

“Benki ya Maendeleo ya Ulaya tumesainiana mkataba sasa ni miezi 24 hawajatoa kibali cha kutupatia fedha, wananiuliza Tanroads ni nani mpaka viwanja vya ndege nimewashajibu  kuwa huu ni  utaratibu  na sera za miundibinu, sasa nashangaa  hawa watu wawakilishi wao wapo hapa nchini wanashindwa kuwataarifu kuhusu sera zetu,”alisema Kamwelwe.

Alisema Serikali ya Tanzania inaomba maafisa wa benki hiyo kuja nchini ili kuangalia uwezo wa Tanroads na kazi wanazozifanya  na waweze kusaini  mktaba huo ambao utasaidia kuboresha miundombinu hiyo nchini.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
167,451FollowersFollow
526,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles