24.7 C
Dar es Salaam
Sunday, November 17, 2024

Contact us: [email protected]

Kisarawe yaja na mkakati mafunzo ya utalii kwa vijana

MWANDISHI WETU-PWANI

Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani,  imeanza mkakati wa kuwaandaa vijana zaidi ya 52 kwa kuwapatia mafunzo ya utalii na kutambua fursa zilizopo katika sekta hiyo ikiwa ni mkakati wa kuinua utalii wilayani humo pamoja na kujiandaa kupokea wageni ambao watakuwa wanapita hapo kuelekea Hifadhi ya Taifa ya Nyerere.

Mafunzo hayo yamefunguliwa leo na Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Jokate Mwegelo, ambapo amesema kuwa vijana ndani ya wilaya hiyo kwa sasa wameamka na wapo tayari kuchangamkia fursa mbalimbali za utalii hasa kwa kuzingatia wamebarikiwa kuwa na kila aina ya vivutio vya utalii.

Amesema kuwa hakuna sababu ya vijana kuendelea kubaki nyuma wakati fursa zipo hivyo wahakikishe kwamba kila wanachokiona Wilayani humo ni fursa niwajibu wao Sasa kuchangamkia fursa hizo.

“Wilaya Kisarawe inafursa kubwa ya utalii kwani inavivutio vingi na ukizingatia Mamlaka ya Hifadhi za Taifa, imepandisha hadhi msitu wa Pugu pamoja na Kazimzumbwi na pia kuna mapango mengi ya utalii hivyo zote hizo ni fursa,” amesema Jokate

Alisema kuwa Kisarawe imekuwa ni chachu ya kuongeza mapato ya halmashauri  hiyo ambapo miaka kadhaa ilikuwa inakusanya Sh bilioni moja  na kwa sasa yamepanda zaidi na kufikia kukusanya Sh bilioni 2.7 kwa mwaka.

Mkuu huyo wa wilaya amempongeza Rais Dk. John Magufuli kwa kuweza kuona umuhimu wa kujenga barabara ya Kisarawe kwenda Hifadhi ya Taifa ya Nyerere kwa kiwango cha lami jambo ambalo sasa litachochea maendeleo kutokana na shughuli za utalii.

Kwa upande wake Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Utalii, Dk. Shogo Sedoyeka amesema  kuwa Kisarawe ni eneo zuri na limejaliwa kuwa shughuli nyingi ikiwamo kuwa lango la utalii kuelekea Hifadhi ya Taifa ya Nyerere.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles