25.2 C
Dar es Salaam
Friday, September 17, 2021

Odama atangaza mapinduzi, filamu yake kuoneshwa Swahiliflix

Jeremia Ernest

Kampuni ya Aflix East Africa kupitia Swahiliflix app kwa kushirikiana na kampuni ya JFILM4 LIFE inayomilikiwa na msanii Jeniffer Kyaka ‘Odama’ wametambulisha filamu mpya ya Kiswahili  iliyopewa jinala Mr.  Kiongozi iliyochezwa na msanii huyo.

Akizungumza na waandishi wa habari leo katika uzinduzi wa Mr. Kiongozi Muwakilishi wa Swahiliflix, Shose Mlay amesema Swahiliflix inawezesha watu mbalimbali kuona filamu za Kiswahili zenye ubora kwa haraka zaidi  hata kwa kutumia simu za viganjani kama naada ya kupakua  Application ya Swahiliflix.

“Ni rahisi sana kuona filamu za Kiswahili kupitia Swahiliflix kwa gharama nafuu ambayo yeyote anaweza kuimudu kwa kua ni rafiki kwa watu wote na mtu huweza kufurahia filamu hata akiwa kwenye daladala au saluni maana hauhitaji kutumia decoder, satellite dishes wala antena,” amesema Mlay.

Aidha Odama alishukuru uongozi wa Swahiliflix kwa kufanya naye kazi katika filamu yake hiyo ambayo inaweza kutazamwa na watu wa rika zote.

“Hii ni frusa kwangu kazi yangu kuonekana dunia nzima nafurahi kwa kua kupitia Mr. Kiongozi jamii itapata elimu inayostahili bila kuchagua umri na jinsia,” anasema Odama.

Hosea Jemba ni mmoja wa waanzilishi wa Swahiliflix, amesema kuwepo kwa  kampuni hiyo kumetoa fursa kwa wadau wa filamu kuonyesha kazi zao duniani kote huku lugha mama Kiswahili ilikendelea kukua na kutangazwa dunia nzima.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
156,520FollowersFollow
517,000SubscribersSubscribe

Latest Articles