26.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Jitihada za rais zaongeza ari ya kulipa kodi mkoani Tanga

Mwandishi wetu, Tanga

WAFANYABIASHARA wa Mkoa wa Tanga, wamesema hawaoni shida
kulipa kodi baada ya kuona utekelezaji wa miradi mikubwa ya maendeleo
inayofanywa na Rais Dk. John Magufuli kupitia kodi zao.


Hayo yalizungumzwa na wafanyabiashara wakati wa kampeni ya elimu
kwa mlipakodi inayoendelea mkoani humo ambako maafisa wa Mamlaka
ya Mapato Tanzania (TRA) kutoka Makao Makuu kwa kukishirikiana na
maafisa wa TRA mkoa wa Tanga.


Maafisa hao waliwatembelea wafanyabiashara kwenye maduka yao
yaliyopo barabara za namba jijini Tanga kwa lengo la kuwaelimisha na
kuwakumbusha kulipa kodi kwa wakati.
Sambamba na hilo, maafisa hao pia waliweza kusikiliza kero
zinazowakabili wafanyabiashara mbalimbali ikiwa ni pamoja na kusikiliza

maoni yao kama mpango wa kutengeneza mazingira rafiki kati yao na
TRA.
Thabiti Salimu ambaye ni mfanyabiashara wa Ukwaju wa jumla na rejareja
katika eneo la barabara za namba amesema kuwa, atamshangaa
mfanyabiashara atayekwepa kulipa kodi hususani katika kipindi hiki
ambacho wameshuhudia miradi mingi ikitekelezwa kupitia kodi zao.


“Rais Magufuli anatumia kodi zetu vizuri, tunaona utekelezaji wa miradi
mingi ya maendeleo hivyo lazima tuendelee kulipa kodi la sivyo kazi ya
utekelezaji wa miradi hii itakwama,” alisema Salimu.


Naye Dina Mbenu, mfanyabiashara wa vipuli vya pikipiki amesema kuwa,
ikiwa wafanyabiashara watakwepa kulipa kodi watasababisha madhara ya
kiuchumi na kuathiri jitihada za serikali za kuboresha miundombinu
ikiwemo barabara.

Amesema hatua ya maafisa wa TRA kuwatembelea kwenye maduka yao
kwa lengo la kuwahamasisha kulipa kodi na kusikiliza kero na maoni yao
inawasaidia kutopoteza muda kwenye ofisi za TRA wakisubiri kuhudumiwa.


Kwa upande wake Afisa Msimamizi Mkuu wa Kodi Julius Mjenga amesema
zoezi la kuwatembelea wafanyabiashara ni endelevu na kabla ya kufanyika
Tanga, zoezi hilo limeshafanyika katika mikoa ya Dar es Salaam, Mwanza,
Mbeya na Morogoro.


Amesema lengo la kufanya hivyo ni kutoa elimu ya kodi, kuwakumbusha
wafanyabiashara kulipa kodi kwa wakati, kusikiliza maoni yao pamoja na
changamoto kwa ajili ya kuzitatua.
Naye Meneja wa TRA Mkoa wa Tanga Specioza Owure, aliwaomba
wafanyabiashara kuunga mkono zoezi linalofanywa na maafisa wa TRA la
utoaji elimu ya kodi, kusikiliza maoni na changamoto zao kwa kuwa zoezi


hilo linalenga kuboresha huduma kwa mlipakodi.
“Niwaombe wafanyabiashara wote mkiwaona maafisa wanatembelea,
msifunge maduka, wapokeeni na kuwapa ushirikiano kwa kuwa wanalenga
kuwaelimisha na kuondoa changamoto mbalimbali zinazowakabili kwenye
biashara zenu ambazo kwa pamoja tunaweza kuzitafutia ufumbuzi,”
alisema Owure.


Amesema zoezi hilo la utoaji wa elimu ya kodi kwa wafanyabiashara
mkoani humo linatarajiwa kumalizika Juni 30, 2020 na kwamba lengo likiwa
ni kutaka kuwafikia wafanyabiashara wengi mkoani hapo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles