23.7 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Kipre Tchetche pasua kichwa

Kipre Tchetche*Azam yaita wanaomtaka wapeleke fedha mezani

*Mwenyewe asema hana mpango na klabu za Bongo

NA SAADA SALIM, DAR ES SALAAM

MSHAMBULIAJI wa Azam FC, Kipre Tchetche, sasa ameanza kupasua vichwa uongozi wa timu yake, lakini uongozi huo umezitaka klabu zinazomtaka waende wakakae nao mezani kuweza kumnunua mchezaji huyo raia wa Ivory Coast.

Juzi Tchetche alitajwa kusaini mkataba wa miaka miwili kwa mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania, Yanga lakini taarifa hizo zilikanushwa kabla ya jana kutajwa pia kusaini klabu ya Al-Nahda Al Buraimi.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Azam, Saad Kawemba, alisema kama kuna klabu zinazotaka kumsajili Tchetche ziwasiliane na uongozi ila si kumsajili kienyeji.

“Tchetche ana mkataba wa mwaka mmoja na zaidi uliobaki, sisi hatuna tabu walete fedha, tunasikia tu wakitamba lakini hatujapokea ofa yoyote hadi sasa na hakuna hata klabu moja iliyotufuata kumnunua.

“Azam haina tabia ya kumzuia mchezaji waje tutamruhusu kwa makubaliano,” alisema Kawemba.

MTANZANIA lilifanya mazungumzo na Tcheche ambaye alikataa kusaini klabu yoyote ile, akisema bado ana mkataba na Azam na hata akiamua kuondoka klabu hiyo hatakuwa na mpango kucheza tena ligi ya Bongo.

“Kama nitaamua kuondoka ninatakiwa kufanya mazungumzo na viongozi wangu, ili waniruhusu kwani bado nina mkataba, imetosha  kucheza Tanzania ninahitaji kwenda kupata changamoto nyingine sehemu nyingine,” alisema.

Mshambuliaji huyo aliyebakiza mkataba wa mwaka mmoja Azam, alisema amecheza soka Tanzania miaka mingi hivyo anahitaji kuondoka katika timu hiyo na kwenda nchi nyingine kujaribu changamoto za maisha ya soka.

Kipre alisema amekuwa na maisha mazuri sana Azam, viongozi na wamiliki wanajali sana wachezaji, lakini nalazimika kuyaacha yote, huu mpango wa kwenda Yanga ni uzushi.

“Hili jambo linanifurahisha nitoke Azam, niende Yanga? Sitaki kuendelea kucheza Tanzania na hadi sasa sijasaini kokote hadi nipewe ruhusa na viongozi,” alisema.

Kipre hakutaka kuweka wazi juu ya nchi wala timu atakayoenda kuchezea.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles