KUALA LUMPUR, MALAYSIA
KIONGOZI wa upinzani wa Malaysia na Naibu Waziri Mkuu wa zamani Ahmad Zahid Hamidi alikamatwa jana na maofisa wa Tume ya Kupambana na Ufisadi.
Kukamatwa kwa Zahid Hamidi kunatokana na  uchunguzi wa matumizi mabaya ya mamlaka, kuvunja uaminifu, na kushiriki utakatishaji wa fedha kupitia wakfu unaohusishwa na familia yake.
Tume hiyo imesema Hamidi atafikishwa mahakamani leo kwa mujibu wa  sheria za kukabiliana na ufisadi na utakatishaji wa fedha.
Hamidi  kiongozi wa chama cha upinzani cha Malay ni miongoni mwa viongozi wa ngazi ya juu kukamatwa baada ya Waziri Mkuu wa zamani, Najib Razak na mke wake, kukamatwa kwa madai kama hayo baada ya kushindwa katika uchaguzi wa Mei.