33.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, November 27, 2024

Contact us: [email protected]

Kinana apokea kilio cha Loliondo

KinanaNA ELIYA MBONEA, NGORONGORO
WANANCHI wa Tarafa ya Loliondo wilayani Ngorongoro mkoani Arusha wameeleza kilio chao cha kuishi kama wakimbizi ndani ya nchi yao kwa Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana.
Kilio hicho walikitoa jana wakati wa mkutano wa hadhara wa Katibu Mkuu uliofanyika mjini Wasso mara baada ya kutembelea utekelezaji Ilani ya uchaguzi na kushiriki shughuli za maendeleo wilayani hapa.
Akizungumza kwa niaba ya wananchi wenzake Lazaro Ngorisa. alimuomba Kinana kuangalia kwa jicho la huruma jambo hilo kutokana na kuishi kwa hofu ya kukimbia makazi yao dhidi ya migogoro na mwekezaji na Hifadhi.
“Hatuna amani, tunawaza kufukuzwa kwa silaha za moto na nyumba zetu kuchomwa kisa mwekezaji anataka kuongeza eneo. Lakini Mamlaka nao wamekuwa wakiongeza mipaka yao kila siku, tunaomba utusaidie,” alisema Ngorisa.
Kwa upande wake Mbunge wa Vijana CCM Mkoa wa Arusha, Catherine Magige naye aliwasilisha kilio cha wananchi wa Loliondo akisema, nyumba za watu zimekuwa zikichomwa kutokana na migogoro ya ardhi isiyoisha.
“Tunaomba utusaidie kumwambia Rais Jakaya Kikwete migogoro ya ardhi iliyopo kati ya wananchi, mwekezaji na hifadhi inawaumiza wanawake na watoto kutokana na nyumba zao kuchomwa moto,” alisema Magige.
Akijibu kilio cha wananchi hao Kinana, alisema mipaka mingi ya hifadhi nchini ilianzishwa miaka ya 1950 wakati idadi ya Watanzania ilikuwa bado ni ndogo, tofauti na ilivyo sasa.
Alisema lipo tatizo linalotokana na migogoro hiyo ya ardhi ambalo husababisha wananchi kupigwa, kuuawa au kuchomewa nyumba pamoja na vyakula.
“Nimeambiwa kila mara mipaka ya hifadhi imekuwa ikiongezwa kwa wananchi. Lakini kuna tatizo la kukamata mifugo au binadamu anapoingia ndani ya Hifadhi wakati mwingine nyumba zinachomwa moto.
“Nani amepewa mamlaka ya kuchoma nyumba, haiwezekani uamke asubuhi uchoma nyumba za watu. Nimewaambia viongozi wa halmashauri waje Dar es nSalaam tukutane na mawaziri wenye dhamana ili watume wataalamu wao kuja kupima upya,”alisema Kinana

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles