MKE wa msanii wa hip hop, Kanye West, Kim Kardashian, ameitaka familia yake kuungana na kaka yao, Rob Kardashian ambaye ametangaza kufunga ndoa mwaka huu.
Rob amekuwa na kipindi kigumu baada ya kumvisha pete mchumba wake, Blac Chyna, ambaye ni mama mtoto wa Tyga.
Tyga kwa sasa ni mchumba wa Kylie Janner, mdogo wa mwisho katika familia hiyo ya Kardashian.
Lakini Kylie alikuwa wa kwanza kumaliza tofauti yake na Rob na kudai kwamba ataungana katika harusi hiyo japokuwa awali alisema ni kitendo cha aibu kutokea kwenye harusi hiyo.
Kim naye ameonyesha kumaliza tofauti na kaka huyo ambapo juzi aliungana pamoja akiwa na wifi yake na kuwataka ndugu wengine wamalize tofauti zao.
“Sioni sababu ya kupoteza undugu wetu kwa ajili ya maamuzi ya mtu, ni vizuri tukaungana pamoja
kwa kuwa wote ni familia moja,” aliandika Kim kwenye akaunti ya Instagram.