25.6 C
Dar es Salaam
Monday, November 25, 2024

Contact us: [email protected]

Kikwete: Wenye vigezo waingizwe TASAF

Na Gustaf Haule, Pwani

NAIBU Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Ridhiwani Kikwete amewataka waratibu wa mpango wa Kunusuru Kaya Maskini (TASAF) kuhakikisha wanaendelea kufanya utambuzi kwa wazee na hata watu wengine wenye vigezo ili waingizwe katika mfuko huo.

Aidha, Kikwete amesema lengo la kuanzishwa kwa TASAF ni kutaka kuwainua watu kutoka katika hali duni ya umaskini na kuwainua kiuchumi ili nao waweze kupata mahitaji muhimu ama ilivyo kwa watu wengine.

Kikwete ametoa kauli hiyo kwa nyakati tofauti alipotembelea miradi mbalimbali ya maendeleo iliyoanzishwa na jamii kupitia TASAF.

Katika ziara hiyo aliyoifanya Julai 11 -12, Kikwete ametembelea mradi wa kilimo cha mbogamboga na matunda katika Kitongoji cha Mwembebaraza Kata ya Janga katika Halmashauri ya Kibaha Vijijini pamoja na vikundi vingine vilivyopo katika kijiji cha Kisanga Kata ya Masaki Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe.

Kikwete amesema kuwa mradi wa TASAF ulianzishwa na Hayati  Benjamini Mkapa kwa ajili ya kuondoa umaskini lakini umeendelee kusaidia jamii mpaka sasa ukiwa chini ya utawala wa Rais Dk. Samia Suluhu Hassan.

Amesema Rais Samia anataka kuona TASAF inaendelea kuwa msaada katika kuwakomboa Watanzania ndiyo maana ameelekeza nguvu nyingi katika mfuko huo na anataka kuona matokeo chanya yanapatikana.

Kikwete ameongeza kuwa kutokana na hali hiyo ni lazima waratibu wa mpango huo kuendelea kufanyakazi ya kuwatambua wazee na wale wote wenye sifa au vigezo vya kuwa katika mpango huo ili nao waweze kusaidiwa.

“Mimi nawapongeza TASAF kwa kazi kubwa na nzuri wanayofanya, maana imewafaidisha wananchi wengi Tanzania lakini Rais Samia anataka kuona kila mwenye sifa ya kuwepo Tasaf anaingizwa ili nao waweze kusaidiwa na mpango huu,” amesema Kikwete.

Kikwete amesema kuwa ni vyema watendaji wa Halmashauri wakaangalia namna ya kushirikiana na Tasaf kwa kuhakikisha zile fedha za asilimia 10 nazo zinaelekezwa katika kuwasaidia watu waliopo katika mpango wa Tasaf kwakuwa wanaweza kulipa mikopo yao.

“Mifuko mingine isaidiane na Tasaf ili kuendelea kuwakwamua kiuchumi watu wenye hali duni maana kuna watu wanakopeshwa fedha mpaka milioni 10 huko Halmashauri lakini kurudisha hawawezi, sasa bora hivi vikundi vya Tasaf vipewe fedha hizo kwakuwa wanaweza kurejesh,” amesema Kikwete.

Makamu mwenyekiti wa Halmashauri ya Kibaha Vijijini, Josephine Gunda amesema Rais Samia amekuwa mkombozi wa jamii ya watu maskini waliopo katika halmashauri yake kwani amewasaidia kubadilika maisha yao.

Mmoja wa wanufaika wa Tasaf kutoka Kitongoji cha Mwembebaraza, Dawia Hassan , ameishukuru serikali kwa kuwapelekea mpango wa Tasaf kwani umemsaidia kusomesha mtoto wake Hassan Kolola mpaka kufikia chuo kikuu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles