Brighiter Masaki
Taasisi isiyo ya kiserikali ya Volunteers in Development imeandaa harambee ya kuchangisha futari kwa ajili ya yatima waishio majumbani kwao na familia zao.
Akizungumza na waandishi wa habari, Mwenyekiti wa Taasisi hivyo, Tune Salimu, amesema mgeni rasmi atakuwa Rais Mstaafu wa awamu ya nne Jakaya Kikwete.
‘’Tumeamua kuunganisha nguvu zetu kuwafikia Yatima na wasiojiweza waishio majumbani kwa kuwa wana changamoto za mahitaji Zaidi ukilinganisha na walewanaoishi kwenye vituo maalum.
“Tuna jumla ya familia 286 zenye Zaidi ya yatima 850 kwenye mikoa mbali mbali bara na visiwani ambayo ni Dar es salaam, Bagamoyo, Mkuranga, Tanga, Arusha, Mwanza na Pemba ’’ amesema Tune Salim, Mwenyekiti wa taasisi hiyo.
Mahitaji ya chakula kwa kipindi cha mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani ni pamoja na, tambi, sukari, tende, maharage, unga wa ngano, unga wa sembe/dona,mafuta ya kupikia, mchele na pamoja na nguo za sikukuu.Kiasi kisichopungua Tsh 54,611,000 kinahitajika ili kuweza kukidhi mahitaji kwa idadi ya watoto hao.
Shughuli hiyo itafanyika leo siku ya jumamosi kuanzia saa 1:00 jioni katika hoteli ya Hyatt Regency Dar es Salaam. Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dk. Jakaya Mrisho Kikwete ndio atakayekuwa mgeni rasmi kwenye shughuli hiyo akifuatana na viongozi wengine wa serikali, viongozi wa kidini, pamoja na wafanya biashara mbalimbali.