25.2 C
Dar es Salaam
Sunday, December 1, 2024

Contact us: [email protected]

Sikwenda nje ya nchi kama mkimbizi wa kisiasa- Mbowe

Na Faraja Masinde, Dar es Salaam

Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) amesema kuwa hakwenda nje ya Nchi kwa sababu za kiasiasa badala yake alikwenda kwa ajili ya kufanua biashara.

Mbowe amebainisha hayo leo, Jumapili Aprili 11, 2021 jijini Dar es Salaam alipokuwa akiongea na waandishi wa Habari.

“Juzi katika mazingira ya kushangaza pengine baada ya kauli za Mama Samia (Rais Samia Suluhu Hassan), TRA wananiandikia barua kwamba ‘zile akaunti zako na zuio la akaunti zako tunazifungua, hivi tu kwamba tumeamua kuondoa zuio la akaunti zako tunazifungua.

“Hamniambii pesa mlizochukua, udharirishaji mlionisababishia, uhuni mliyonifanyia, sasa ni wafanyabiashara wangapi, na ndiyo sababu moja wapo ndugu zangu Watanzania iliyonisababisha niondoke nchini.

“Sikwenda nchi za nje kama mkimbizi wa kisiasa bali kutafuta uwekezaji katika mataifa mengine, siyo kwamba sikuweza kufanya biashara nchini Tanzania kila biashara niliyojaribu kuifanya Tanzania ilizuia, ilifungiwa, iliharibiwa ilifungiwa, kwa hiyo nikaona naweza kufanya biashara Dubai,” amesema Mbowe.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles