29.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

Kikosi kipya Chadema 2015

Kikosi cha Chadema
Kikosi cha Chadema

NA SHABANI MATUTU, DAR ES SALAAM

HATIMAYE Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeunda kikosi kazi cha kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015, baada ya makada nane kuchaguliwa na Baraza Kuu kuwa wajumbe wa Kamati Kuu.

Katika kikosi hicho, Mbunge wa Ubungo, John Mnyika amevaa viatu vya aliyekuwa Makamu Katibu Mkuu wa chama hicho Bara, Zitto Kabwe.

Safu ya kikosi hicho ambacho kitaongozwa na Mwenyekiti Freeman Mbowe, ilikamilika juzi usiku kwa Baraza Kuu kuchagua wajumbe nane wa Kamati Kuu, ikiwamo kuthibitisha uteuzi wa viongozi wa Kamati Tendaji kwa Bara na Zanzibar.

Katika safu ya Kamati Tendaji, mbali na Mnyika, chama hicho kimemteua mwanahabari, Salum Mwalimu Juma, kuwa Naibu Katibu Mkuu Zanzibar, huku  nafasi ya Katibu Mkuu ikirudi kwa Dk. Willibrod Slaa.

Kwa upande wa wajumbe wa Kamati Kuu Bara, wanamume, waliorejea ni Profesa Mwesiga Baregu aliyepata kura 127 na Mabere Marando (164).

Sura mpya zilizoingia kwenye Kamati Kuu  Bara ni  Dk. Yared Fubusa aliyepata kura 127 na kwa upande wa Zanzibar, ilikwenda kwa Salum Mwalim Juma (112).

Wajumbe wa Kamati Kuu wanawake Bara, ilichukuliwa na sura mpya Catherine Vermand (97) na Suzan Kiwanga (93), wakati upande wa Zanzibar nafasi hiyo ilikwenda kwa Zainabu Musa Bakari (111) ambaye pia ni mpya.

Kazi ya kuchagua wajumbe nane ilihitimishwa kwa kuchaguliwa Elly Marco Macha kupitia nafasi ya watu wenye ulemavu iliyokuwa ikishikiliwa na marehemu mama mzazi wa Zitto, Shida Salum.

MAKAMU WENYEVITI
Nafasi ya Makamu Mwenyekiti Bara imechukuliwa na Profesa  Abdallah Safari na kwa Zanzibar ni Said Issa Mohammed.

BARAZA LA WAZEE
Mwenyekiti wa baraza hilo, amechaguliwa Hashim Juma Issa, makamu wake ni Susan Lyimo, wakati  Makamu Mwenyekiti  Zanzibar ni Omar Masoud Omar, huku nafasi ya Katibu Mkuu ikienda kwa Rodrick Lutembeka.

BAWACHA
Nafasi ya Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake Chadema (BAWACHAa) ilikwenda kwa Halima Mdee na nafasi ya Makamu Mwenyekiti Bara ilichukuliwa na Hawa Mwaifunga, huku Makamu Mwenyekiti wa Zanzibar akiwa Hamida Abdallah.

BARAZA KUU BAWACHA
Nafasi hiyo kwa Zanzibar ilichukuliwa na Janeth Medadi Fusi, huku kwa upande wa Bara ilichukuliwa na mwandishi wa habari wa Gazeti la Tanzania Daima, Janeth J. Mjungu, Restuta Said Mjoka, Marietha Cosmas Chenyenge na Suzan Kiwanga.

BAVICHA
Nafasi ya Mwenyekiti  wa Baraza la Vijana Chadema (BAVICHA) ilikwenda kwa Paschal Patrobas na nafasi ya Makamu Mwenyekiti Bara ilikwenda kwa Patrick Sosopi na kwa upande wa Zanzibar, alichaguliwa Zeudi M. Abdallah.

VIGOGO WALIOANGUSHWA
Baadhi ya vigogo walioangushwa katika uchaguzi huo kwenye nafasi mbalimbali ni pamoja na Fred Mpendazoe, mwanaharakati Hebron Mwakagenda, aliyekuwa Katibu wa BAVICHA, Deogratius Mushi, Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Iringa, Chiku Abwao, Mhariri Mtendaji wa Tanzania Daima, Ansbert Ngurumo, Mwenyekiti Mkoa wa Kinondoni, Henry Kilewo na Dk. Arcado Ntagazwa.

- Advertisement -

Related Articles

1 COMMENT

  1. Ongera CHADEMA kupata safu mpya ya uongozi sasa ni kazi kwenda mbele. Ni wakati wa kusema vitisho vya polisi basi. Tangaza na tayarisha maandamano, tuandamane ili polisi waue wale tu ambao tarehe yao itakuwa imefika na tutaobaki tuendeleze mapambano mpaka nchi yetu izaliwe mara ya pili.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles