27.2 C
Dar es Salaam
Sunday, November 24, 2024

Contact us: [email protected]

Kihenzile  aitaka TCAA kusimamia ubora wa miradi

Na Esther Mnyika, Mtanzania Digital

Naibu Waziri wa Uchukuzi, David Kihenzile, ameitaka

Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Anga (TCAA), kuhakikisha wanasimamia  ubora wa miradi ili imalizike kwa wakati.

Kauli hiyo ameitoa leo Novemba 22, 2023 jijini Dar es Salaam, alipotembelea  Ofisi  za  mamlaka  hiyo  kwa  lengo la kufahamiana na kupata fursa  ya kuonana na Menejimenti  na kujua mpango wa wafanyakazi wake.

Kihenzile  amesema  haikubaliki mradi wa mwaka mmoja unashindwa  kumalizika kwa wakati uliopangwa.

“Muendelee kusimamia ubora  wa miradi hii iweze kukamilika kwa wakati na thamani ya fedha  zilizotolewa,  muweke utaratibu  mzuri wa kusimamia maelekezo  yaliyotolewa na viongozi  yawe na mfumo  wa utekelezaji,” amesema Kihenzile.

Ameagiza pia TCAA kusimamia  mashirika  yao ya ndege ya ndani na nje ili kudhibiti ajali  na  kutafuta ufumbuzi wa malalamiko ya wananchi ikiwamo kuahirisha  safari.

“Zaidi ya  mabilioni yameelekezwa  katika miradi na  bado Rais Dk. Samia Suluhu Hassan anatenga fedha ili kuhakikisha usalama wa vifaa vya mbalimbali vya angani ambavyo kimsingi vina dhibitiwa na vina simamiwa na TCAA,”amesema.

Aidha amesema ipo miradi kadhaa  mikubwa ambayo inafanyika  kati yake ni  ujenzi wa chuo cha usafiri wa anga ambacho kinafundisha watu mbalimbali.

“Tumeelezwa katika vyuo tisa bora barani Afrika cha TCAA  ni mojawapo na duniani vipo 35 tu. Rais Dk .Samia  anapanga utaratibu wa kutenga fedha ili kuendelea kuwekeza zaidi kujenga chuo cha kisasa kama anavyofanya kwenye sekta nyingine,” ameeleza.

Kihenzile  ametoa wito kwa mashirika, wawekezaji, wafanyabiashara  waingie kwenye usafiri  huo, kwa kuwa  ndani nan je ya nchi usafiri wa anga ni salama.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Anga  (TCAA),Hamza Johari, amesema  naibu waziri huyo ameridhishwa na kazi ambazo wanafanya.

“Naibu Waziri ametoa maelekezo ikiwemo  katika suala zima la miradi  kuhakikisha kwamba wanafanya miradi hiyo kwa viwango na ubora unatakiwa na inamalizika kwa wakati,” amesema Johari.

Amesema  miradi  wanayoendelea nayo kwa sasa ni  wa kubadilisha mifumo ya sauti, kuboresha mawasiliano na mradi wa ujenzi  wa chuo cha usafiri wa anga.

Amesema katika miradi  hiyo yote mitatu  watahakikisha  maelekezo  waliyopewa yatayafanyia ili kufikia viwango vya kimataifa.

Aidha amesema  katika kuongeza mashirika ya ndege, wanaamini  itasaidia na gharama za nauli zinapungua.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles