33.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, November 27, 2024

Contact us: [email protected]

Kigogo TEA, wafanyakazi benki wasomewa mashtaka 400

NA MWANDISHI WETU

ALIYEKUWA Mhasibu Mwandamizi wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), Isaya Philip (39) na watumishi wengine 11 wa Benki ya CRDB, wamefikishwa katika Mahakama ya Wilaya Kinondoni, wakikabiliwa na mashtaka 404 likiwemo la kuisababishia Serikali hasara ya zaidi ya Sh milioni 569.

Katika mashitaka waliyosomewa ya kughushi ni 189, ya wizi 145, kuwasilisha nyaraka za uongo79, kula njama ya kutenda kosa moja na kusababisha hasara moja.

Akisoma hati ya mashtaka wakili wa Serikali kutoka Taasisi ya Kuzuia na kupambana na Rushwa (Takukuru),  Faraja Sambala akisaidiana na Heri Mchome, mbali na  Philip aliwataja washtakiwa wengine kuwa ni Tehan Spendy, Jones Lisso, Adelphine Barongo, Daniel Kahamba, Benedicta Boniface, Edina  Rwiza, Ally Hamad, Msafiri Sobo, Anthony Moshi, Aisha Mussa na Khaji Selemani.

Washtakiwa hao waliosomewa mashtaka hayo mahakamani hapo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Frank Moshi, wanadaiwa kutenda makosa hayo kati ya mwaka 2010 na 2013 na wameshtakiwa chini ya sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa namba 11/2007 na sheria ya kanuni ya adhabu sura ya 16 na sheria ya uhujumu uchumi sura ya 200 kama zilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2002.

Katika shtaka la 403 mshtakiwa Philip anadaiwa kwa njia isiyo ya uwaminifu, aliisababishia TEA hasara ya zaidi ya Sh. milioni 569 ambapo inadaiwa alitenda kosa hilo Oktoba mosi 2010, na Februari 28, 2013.

Katika Shtaka la 404, linalowakabili washtakiwa wote wanadai kuwa Oktoba Mosi, 2010, na Februari 28, 2013 katika ofisi za TEA waliisababishia Serikali hasara ya zaidi ya Sh milioni 569.

Hata hivyo washtakiwa hao wamekana kutenda makosa hayo, huku upande wa mashtaka ukidai kuwa upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika.

Wakili wa utetezi Majura Magafu, aliomba washtakiwa hao wapewe dhamana kwa kuwa mashtaka yanayowakabili yanadhaminika.

Hakimu Moshi aliahirisha kesi hiyo hadi Oktoba 10, mwaka huu kwa ajili ya kutoa uamuzi kuhusu dhamana ya washtakiwa isipokuwa mshtakiwa wa kwanza ambaye alipewa dhamana katika Mahakama Kuu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles