28.7 C
Dar es Salaam
Friday, May 24, 2024

Contact us: [email protected]

KIGOGO ESCROW ARUHUSIWA KWENDA KUTIBIWA

Na SANGU JOSEPH (TUDARCO)

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam, imeamuru Mmiliki wa Kampuni ya Kufua Umeme ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL), Harbinder Singh Seth, aende kutibiwa kutokana na matatizo ya kiafya yanayomsumbua.

Amri hiyo imekuja baada ya Seth kusimama mbele ya mahakama hiyo jana wakati shauri lake likiendelea na kudai kuwa ana matatizo ya kiafya na kuomba apewe kibali ili aweze kutibiwa.

Kutokana na hali hiyo, Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shahidi, aliitaka Serikali kumpeleka hospitali ili aweze kupatiwa matibabu kutokana na maradhi hayo.

 

Hakimu Shahidi aliahirisha shauri hilo hadi Agosti 3, mwaka huu, kwa ajili ya kutajwa tena. Julai 14, mwaka huu, upande wa utetezi, ukiongozwa na Wakili Alex Balomi, uliieleza mahakama hiyo kuwa mteja wao anahitaji kupewa mtaalamu wa afya kwa sababu ana uvimbe tumboni kama puto, pia anakosa usingizi.

 

Awali, washtakiwa hao walipandishwa kizimbani na kusomewa mashtaka sita, yakiwamo kula njama, uhujumu uchumi, kujihusisha na mtandao wa uhalifu, kutoa nyaraka za kughushi, kujipatia fedha kwa njia za udanganyifu na kuisababishia Serikali hasara ya zaidi ya Sh bilioni 300.

Wakati kesi hiyo inaendelea, Julai 3, mwaka huu, vigogo hao walisomewa hati nyingine mpya ya mashtaka mengine sita yanayofanana na yale ya awali, yakiwamo matano ya kutakatisha fedha na moja la kuhamisha fedha.

Wanadaiwa kuwa, kati ya Oktoba 18, 2011 na Machi 19, 2014 jijini Dar es Salaam, walikula njama katika nchi za Afrika Kusini, Kenya na India ya kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.

Katika shtaka la kujihusisha na mtandao, washtakiwa hao wanadaiwa kuwa kati ya Oktoba 18, 2011 na Machi 19, 2014, jijini Dar es Salaam, wakiwa si watumishi wa umma na watumishi wa umma,  walitekeleza mtandao huo wa uhalifu kwa lengo la kujipatia faida.

Kwa upande wa Seth, anadaiwa kuwa   Oktoba 10, 2011, katika Mtaa wa Ohio, Ilala, jijini Dar es Salaam, akiwa na nia ya ulaghai, alighushi fomu namba 14 ya usajili wa kampuni na kuonesha yeye ni Mtanzania anayeishi kitalu namba 887, Masaki, wakati akijua ni uongo.

Pia Sethi anadaiwa kughushi fomu namba 14 ya usajili wa kampuni kwa Ofisa Msajili wa Kampuni, Seka Kasera, kwa njia ya kuonyesha kwamba yeye ni Mtanzania na mkazi wa Mtaa wa Mrikau.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles