25 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

Kifo cha Kristina chamfikisha Nick Gordon mahakamani

nick-gordon2--zGEORGIA, Marekani

ALIYEKUWA mpenzi wa marehemu Kristina Brown, Nick Gordon, amekana kuhusika na kifo cha aliyekuwa mpenzi wake mtoto wa Bobby Brown na marehemu Whitney Houston, Kristina Brown.

Kristina alifariki Julai 26 baada ya kuanguka akiwa bafuni Januari 31 mwaka huu na Gordon kuhusishwa na kifo hicho kutokana na kuwa na marehemu mara ya mwisho kabla ya kupatwa na ugonjwa huo.

Vipimo vilivyopimwa vya mwanadada huyo vimeonyesha aliwekewa sumu kwenye kinywaji chake na Gordon ndiye anayetuhumiwa kuhusika na tukio hilo.

Juzi Gordon alifikishwa mahakamani na kushtakiwa kwa kosa hilo, lakini alikana kuhusika na kifo hicho.

Mtandao wa TMZ umeripoti kuwa Gordon ana wakati mgumu na familia ya Kristina kwa kuwa inaonekana kuendelea kumfuatilia zaidi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles