22.8 C
Dar es Salaam
Wednesday, May 22, 2024

Contact us: [email protected]

50 Cent: Sijafilisika na sifilisiki ng’o

50NEW YORK, Marekani

BAADA ya tetesi kwamba msanii wa hip hop nchini Marekani, Curtis Jackson ‘50 Cent’ amefilisika, msanii huyo ameibuka na kuweka wazi baadhi ya vitu anavyojenga kwa sasa akionyesha kwamba bado ana hazina kubwa ya fedha.

Hivi karibuni alionyesha nyumba yake mpya ambayo ameijenga barani Afrika lakini hajasema iko nchi gani.

Kupitia akaunti yake ya Instagram, msanii huyo amesema alitangaza kufilisika akiwa na lengo la kujiimarisha kibiashara kwa kujilinda na waovu.

“Bado nipo vizuri katika biashara, sijafilisika kama watu wanavyodhani ila nilifanya hivyo kwa ajili ya kujilinda katika biashara zangu,” alisema 50 Cent ambaye anahisa nyingi katika makampuni mbalimbali ya mavazi, vinywaji, ngumi na uchimbaji madini.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles