30.2 C
Dar es Salaam
Thursday, May 23, 2024

Contact us: [email protected]

Kidato cha nne kuanza mtihani leo

pg-25Na JONAS MUSHI-DAR ES SALAAM

BARAZA la Mitihani Tanzania (NECTA) limeonya wanafunzi, wasimamizi na walimu watakaohusika katika udanganyifu wa mitihani ya taifa ya kidato cha nne inayoanza leo  nchini kote.

Akizungumza  Dar es Salaam jana, Katibu Mtendaji wa NECTA, Dk. Charles Msonde, alisema Bazara halitamvumilia mtu yeyote atakayebainika kushiriki vitendo vya udanganyifu kwa sababu  atachukuliwa hatua za  sheria na  nidhamu.

Alisema maandalizi yote ya mitihani yamekwisha kukamilika ikiwa ni pamoja na kusambaza mitihani, vijitabu vya kujibia na nyaraka zote muhimu katika mikoa yote ya Tanzania bara na Visiwani.

Dk. Msonde alizitaka kamati za mitihani za mikoa, halmashauri na manispaa kuhakikisha taratibu za mitihani ya taifa zinazingatiwa.

Alisema   wanafunzi watakaobainika kufanya vitendo vya udanganyifui watafutiwa matokeo yao yote na   walimu na wasimamizi watachukuliwa hatua za sheria na kanuni za utumishi wa umma.

“Baraza la Mitihani Tanzania linawaasa wanafunzi, walimu na wanachi wote kwa ujumla kutojihusisha na na vitendo vyovyote vya udanganyifu wa mtihani huu.

“Hatutasita kumchukulia hatua yeyote atakayebainika kwa mujibu wa kanuni za utumishi wa umma na sheria za nchi,” alisema Dk. Msonde.

Alisema  watahiniwa 408,442  wamesajiliwa kufanya mtihani huo na kati yao watahiniwa wa shule ni 355,995 na wa kujitegemea ni 52,447.

Alisema kati ya watahiniwa wa shule 355,995 waliosajiliwa, wavulana ni 173,423 (asilimia 48.72) huku wasichana wakiwa 182,572 (asilimia 51.28) na kati yao watahiniwa 59 ni wasioona na 283 wenye uoni hafifu.

Kwa   watahiniwa 52,447  wa kujitegemea,   wanaume ni 25,529 (asilimia 48.68) na wanawake ni 26,918 (asilimia 51.32) na  miongoni mwao wapo wasioona saba wanawake wakiwa watatu na wanaume wanne.

Kuhusu mtihani wa maarifa (QT), alisema watahiniwa 20,634 wamesajiliwa kufanya mtihani huo mwaka huu ambako wanaume ni 7,819 (asilimia 37.89) na wanawake ni 12,815 (asilimia 62.11).

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles