28.4 C
Dar es Salaam
Friday, February 23, 2024

Contact us: [email protected]

Kiboko na mkewe jela miaka 20

Na Kulwa Mzee, Dar es Salaam

Mfanyabiashara, Ayubu Kiboko na mkewe Pili Kiboko wametiwa hatiani na kuhukumiwa kwenda jela miaka 20 kila mmoja kwa kosa la kukutwa na dawa za kulevya aina ya heroine.

Washtakiwa hao wametiwa hatiani leo jioni Desemba 18, na Mahakama Kuu Kitengo cha Rushwa na Uhujumu Uchumi mbele ya Jaji Lilian Mashaka.

Mawakili wa Serikali walioendesha kesi hiyo. Salim Msemo na Constantine Kakula walileta Mashahidi 6 na vielelezo 16 huku upande wa utetezi wakitetewa na Nehemia Nkoko na Majura Magafu walikuwa na mashahidi wawili pamoja na vielelezo 2.

Katika kufikia uamuzi mahakama ilijikita katika hoja nne ambapo hoja ya kwanza ni iwapo unga ndani ya mfuko mweusi wa naylon ambao ni kielelezo P.11a na P.11b ni dawa za Kulevya?

Mbili iwapo upekuzi ulifanyika ndani ya nyumba ya watuhumiwa na vielelezo P.11a na P.11b vilikutwa ndani ya nyumba ya watuhumiwa.

Hoja ya tatu iwapo mnyororo wa utunzaji wa kielelezo ulikatika na nne iwapo kesi ya upande wa utetezi ulileta mashaka kwenye kesi ya upande wa Jamhuri.

“Kutokana na hoja hizo na ushahidi uliotolewa upande wa mashtaka kwa ujumla umethibitisha kosa la kusafirisha dawa za kulevya aina ya Heroine Hydrochloride hivyo Mahakama imewatia hatia washtakiwa wote kwa kosa la kusafirisha dawa hizo,”.

Upande wa Jamuhuri wameomba adhabu kali kwasababu dawa zina madhara mbali mbali kwa watu wakiwemo vijana, na fedha zinazopatikana sio halali na imekuwa ikiathiri Uchumi wa uwepo wa fedha haramu ambazo zinamadhara kwenye Uchumi wa nchi yetu.

Pia iwe fundisho kwa watu wengine wenye tabia hizo waweze kuacha na wasiingie katika biashara hiyo.

Upande wa utetezi waliomba kwamba washtakiwa wapunguziwe adhabu ni wazazi na wana watoto na toka walipokamatwa hadi leo wanajiendesha wenyewe mmoja ana umri wa miaka 14.

Mahakama pia izingatie kuwa hawana rekodi yoyote ya makosa ya jinai
Izingatie walikuwa wanafanya shughuli zilizokuwa halali na hakuna ushahidi uliotolewa kuonyesha kuwa kipato chao kilitokana na biashara ya dawa za Kulevya. Mahakama pamoja na kuzingatia hoja hizo iliwahukumu kifungo cha miaka 20 kila mmoja na dawa ziteketezwe.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles