25.9 C
Dar es Salaam
Thursday, December 19, 2024

Contact us: [email protected]

KIBAKI AMPIGIA KAMPENI MPWA WAKE

NAIROBI, KENYA


RAIS mstaafu wa Kenya, Mwai Kibaki, ameonekana kurudi katika siasa za eneo la Mlima Kenya akimpigia kampeni mpwa wake licha ya kukiri hayuko sawa kiafya.

Kibaki alijitokeza katika ulingo huo kumfanyia kampeni mpwa wake huyo Nderitu Muriithi, ambaye anawania ugavana wa Kaunti ya Laikipia kwa tiketi ya chama cha Jubilee.

Katika hotuba yake ya dakika 20 akiwa Uwanja wa Michezo wa Klabu ya  Nanyuki, Kibaki aliwahutubia wajumbe 300 waliokusanyika hapo.

Aliwaambia kuwa ana maumivu ya shingo, ikiwa ni miezi kadhaa baada ya kurudi nyumbani kutoka matibabu Afrika Kusini ambako alikuwa amelazwa kwa matatizo ya damu kuganda.

Agosti mwaka jana, Kibaki aliyelazwa katika Hospitali ya Netcare Sunninghill nchini humo ili kuondoa damu iliyoganda katika mshipa wa shingoni, alisema anaweza kuongea kwa sauti.

Wakati wa mkutano huo alisifu mpango wa maendeleo uliowasilishwa na Muriithi kwa ajili ya eneo hilo kame na kumtaja kuwa mwanamume mwenye bidii.

Aidha siku ya Ijumaa, alifanya mkutano kama huo wa kisiasa mjini Nyahururu.

Hii ni mara ya kwanza kwa Kibaki kushiriki siasa za eneo hilo tangu mwaka 2013 alipoondoka madarakani na hakuna yeyote miongoni mwa wana familia yake, aliyejitokeza kuwania wadhifa wa siasa.

“Wanaofanya kazi kwa bidii hupendwa wakati wote. Nina ujuzi katika mambo haya na nimekuwa hapo. Ninaamini tutafaulu na kupata kazi,” alisema Kibaki akimuunga mkono waziri msaidizi huyo wa zamani wa viwanda.

Alitoa mwito kwa wananchi kuzingatia zaidi sekta za maji na miundomsingi akiongeza kuwa ushirikishi wa umma ni muhimu pia katika uongozi.

“Maji ni muhimu sana na usiseme tu, bali yashughulikie. Tafuta njia za kuongeza upatikanaji wa maji,” alisema Kibaki ambaye ni mjumbe maalum wa Maji wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO).

Murithi atachuana na gavana wa sasa Joshua Irungu na amemchagua John Mwaniki aliyekuwa rafiki wa gavana kabla ya kufarakana kuwa mgombea wake mwenza.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles