28.7 C
Dar es Salaam
Monday, October 25, 2021

MAPOROMKO YA ARDHI YAUA WATU 250 COLOMBIA

BOGOTA, COLOMBIA


JESHI la Colombia limesema idadi ya waliokufa kutokana na maporomoko ya ardhi nchini hapa imefikia watu 250 huku waliojeruhiwa wakiwa 400.

Hata hivyo, idadi hiyo huenda ikaongezeka kwa vile bado kuna zaidi ya watu 200 ambao hawajulikani walipo.

Vikosi vya uokoaji vinavyoendesha shughuli hizo vinasema nyingi ya barabara za eneo lililotokea maporomoko hayo katika mji wa kusini wa Mocoa hazipitiki.

Maporomo hayo yametokea baada ya mvua kubwa kunyesha kwa saa nyingi.

Viongozi wa mataifa jirani wa Mexico na Argentina walikuwa wa kwanza kutoa ujumbe wa pole na kuahidi kuisaidia Colombia.

Rais Juan Manuel Santosa alitangaza hali ya tahadhari eneo hilo na alisafiri kwenda kukagua maendeleo ya shughuli za uokoaji.

Picha zilizochapishwa kwenye mitandao na jeshi zilionyesha baadhi ya majeruhi wakiokolewa kwa ndege.

Katika miezi ya hivi karibuni eneo hilo limekuwa likikumbwa na maporomoko ya ardhi.

Novemba mwaka jana, watu tisa walikufa kwenye mji wa El Tambo, karibu kilomita 140 kutoka Mocoa kufuatia maporomoko ya ardhi yaliyosababiswa na mvua kubwa.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
163,085FollowersFollow
522,000SubscribersSubscribe

Latest Articles