33.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, November 27, 2024

Contact us: [email protected]

Kiama Wachinga Ilala leo

machingaNa HADIA KHAMIS- DAR ES SALAAM

WAFANYABIASHARA wanaopanga bidhaa zao kando kando ya barabara ya mwendokasi na Kivukoni Feri, wametakiwa kuhama maeneo hayo na kwenda kutafuta maeneo maalumu yaliyotengwa kufanya biashara hizo.

Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema, alisema ni vyema wafanyabiashara hao waondoke wenyewe bila ya kulazimishana.

Mkuu huyo wa wilaya aliwataka askari wa jiji kuhakikisha wafanyabiashara hao hawaendelei kufanya biashara katika maeneo hayo.

Alisema leo atahakikisha biashara zote zinazowekwa kwenye barabara ya mwendo kasi au kando ya barabara ya watembea kwa miguu zinaondolewa na kupelekwa Halmashauri ya jiji hilo.

“Kwa Feri pekee wapo wafanyabiashara zaidi ya 35 ambao watapangiwa sehemu maalumu ya kufanya ikiwa ni pamoja na kupewa vizimba katika masoko.

Alisema kitendo cha wafanyabiashara hao kufanya biashara kandokando ya barabara ni kinyume cha sheria ya mazingira za Jiji la Dar es Salaam.

“Kila sehemu kuna utaratibu na sheria zake, hakuna sheria inayoruhusu wafanyabiashara kufanya biashara kando kando ya barabara, lakini wafanyabiashara wanavunja sheria kwa kuuza biashara zao maeneo haya,” alisema Mjema.

Alisema kwa Manispaa ya Ilala yapo masoko mengi ya wafanyabiashara ndogo ndogo hivyo ni vyema kwenda katika maeneo yaliyotengwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles