27.9 C
Dar es Salaam
Monday, June 24, 2024

Contact us: [email protected]

KESI YA WEMA YAPIGWA KALENDA

PATRICIA KIMELEMETA NA MANENO SELANYIKA

 

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu inatarajia kutoa uamuzi mdogo wa ushahidi unaomhusu aliyekua Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu.

Kauli hiyo imetolewa jana na Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba wa mahakama hiyo, ambapo alisema uamuzi huo ulipaswa kutolewa jana, lakini ilishindikana baada ya kuchelewa kuandika.

 

Alisema alipaswa kwanza kufanya utafiti wa kina kuhusiana na ushahidi unaolalamikiwa ili aweze kutoa uamuzi stahiki.

 

“Nimekaa na mawakili wa pande zote mbili ili kujadiliana suala hili kabla sijatoa uamuzi, lakini pia napaswa kufanya utafiti ili niweze kujiridhisha na suala linalobishaniwa,” alisema Hakimu Simba.

 

Alisema kutokana na hali hiyo, uamuzi wa suala hilo utatolewa Agosti 31, mwaka huu na kesi ya msingi itaendelea kusikilizwa Septemba 12 na 13 mwaka huu.

 

Awali katika kesi hiyo, wakili anayemtetea Wema, ambaye pia ni Rais wa TLS, Tundu Lissu, aliiomba mahakama hiyo kutopokea kielelezo cha ushahidi wa msokoto mmoja na vipisi viwili vya bangi vinavyodaiwa kukutwa nyumbani kwa Wema.

 

Lissu amepinga kielelezo hicho, mbele ya hakimu huyo baada ya wakili wa Serikali, Costantine Kakula, kumuongoza shahidi wa kwanza wa upande wa mashtaka, ambaye ni Mkemia kutoka Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Elias Mulima.

 

Lissu amedai kuwa, kielelezo cha ushahidi kisipokelewe kwa sababu ndani ya bahasha yenye ushahidi kuna vitu zaidi ya msokoto mmoja na vipisi viwili vinavyodaiwa kuwa ni bangi.

 

Lissu amedai vipisi viwili vyenyewe ni majani ambayo akiviangalia kwa makini ni vipisi vya sigara za kienyeji ambazo zimetumika kwa sababu vina alama ya kuungua ambavyo kwao vinaitwa twagooso.

 

Wema na wafanyakazi wake wawili, Matilda Abbas na Angelina Msigwa walipandishwa kizimbani Februari, mwaka huu na kusomewa mashtaka, likiwamo la kukutwa na kutumia dawa za kulevya aina ya bangi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles