Na Kulwa Mzee, Dar es Salaam
Kesi ya matumizi mabaya ya madaraka inayomkabili Mkurugenzi Mkuu wa zamani wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Tido Mhando itaanza kusikilizwa Machi 28, mwaka huu.
Hayo yamebainishwa leo katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu baada ya mshtakiwa kusomewa maelezo ya awali mbele ya Hakimu Mfawidhi wa mahakama hiyo, Victoria Nongwa.
Katika maelezo hayo ya awali, Tido alikubali maelezo yake binafsi, alikubali alikuwa Mkurugenzi  Mkuu wa TBC kuanzia mwaka 2006 hadi 2010.
Alikubali alikuwa msimamizi katika shughuli za TBC lakini siyo kwa shughuli zote.
Pia kutoka maelezo katika Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), lakini hakukiri na kuwa alifikishwa mahakamani Januari 26, mwaka huu. Hata hivyo Tido aliyakana mashtaka yote dhidi yake.