28.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

KESI YA MBOWE, DC KUENDELEA SEPT. 5

Na UPENDO MOSHA-MOSHI

MAOMBI ya kuunganishwa kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali katika kesi inayomkabili Mkuu wa Wilaya (DC) ya Hai, Gelasius Byakanwa, katika Mahakama Kuu, Kanda ya Moshi, yanatarajia kuanza kusikilizwa Septemba 5.

Byakanwa ameshtakiwa na Kampuni ya Kilimanjaro Veggies Ltd inayomilikiwa na Mbunge wa Hai, Freeman Mbowe.

Kesi hiyo ambayo inasikilizwa na Jaji Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Aishael Sumari, iliahirishwa baada ya jaji huyo kukabiliwa na jukumu jingine la kusikiliza kesi za dawa za kulevya zilizokuwa zikiendelea mahakamani hapo.

“Kesi hii naiahirisha hadi Septemba 5, mwaka huu, kwa kuwa mheshimiwa jaji anayesikiliza kesi hii, ana majukumu mengine ya kusikiliza kesi za dawa za kulevya.

“Kwa hiyo, hiyo Septemba 5, shauri hili litasikilizwa majira ya saa tatu kamili asubuhi,” alisema Naibu Msajili wa Mahakama Kuu, Kanda ya Moshi, Bernad Mpepo alipokuwa akiahirisha shauri hilo.

Hatua hiyo ya kumjumuisha Mwanasheria Mkuu wa Serikali katika kesi hiyo, imekuja baada ya Modestus Njau ambaye ni wakili anayemtetea mkuu wa wilaya hiyo, kuiomba mahakama kuona umuhimu wa kumjumuisha kwa kuwa Byakanwa ni mtumishi wa umma na alikuwa akitekeleza majukumu ya Serikali yaliyosababisha afunguliwe kesi mahakamani.

Katika kesi hiyo, Kampuni ya Kilimanjaro Veggies Ltd inawakilishwa na wakili wa  Kampuni ya Uwakili ya D’Souza & Co ya jijini Arusha, Meirad Souza.

Juni 30 mwaka huu, Kampuni ya Uwakili ya D’ Souza kwa niaba ya Kampuni ya Kilimanjaro Veggies Ltd, ilimfungulia kesi mkuu huyo wa wilaya pasipo kuihusisha Serikali.

Katika shauri hilo, Byakanwa anadaiwa fidia ya zaidi ya Sh milioni 549.3 kutokana na kuharibu na kuondoa mindombinu ya umwagiliaji katika shamba la kampuni hiyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles