26.3 C
Dar es Salaam
Wednesday, November 27, 2024

Contact us: [email protected]

KESI YA KUPINGA SHERIA YA HUDUMA ZA VYOMBO VYA HABARI YAANZA KUUNGURUMA EALA

Na Eliya Mbonea, Arusha

Mahakama ya Afrika Mashariki (EALA), imeanza kusikiliza kesi ya kupinga Sheria ya Huduma za Vyombo vya Habari ya mwaka 2016 iliyofunguliwa na Baraza la Habari Tanzania (MCT), wakishirikiana na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) pamoja na Muungano wa Asasi zinazotetea haki za Binadamu (THRDC).

Leo Jumanne Machi 13, mahakama hiyo imesikiliza makubaliano ya msingi ya kesi hiyo namba2, ya mwaka 2017 inayopinga baadhi ya vifungu vya Sheria ya huduma ya Vyombo vya habari ya Mwaka 2016.

Mbele ya Jopo la Majaji wa Mahakama ya EALA, wakiongozwa na Jaji Kiongozi Monica Mugenyi, Faustini Ntezilyayo na Fakhi Jundu waleta na wajibu maombi walikubaliana kufanyia kazi baadhi ya hoja kabla ya Mei 28, mwaka huu.

Pande hizo mbili katika shauri hilo zilikubaliana kwamba Aprili 13, waleta maombi watawasilisha malalamiko yao, ambapo Mei 14, wajibu maombi watajibu hoja za walalamikaji, huku Mei 28, waleta maombi endapo watakuwa na jambo la ziada wataruhusiwa kuongeza.

Katibu Mtendaji wa MCT, Kajubi Mukajanga akizungumza nje ya Mahakama hiyo amesema, “Sheria hii kwa maoni yetu inaminya uhuru wa wananchi kupata habari kwa kuweka vikwazo ambavyo havina sababu kwani vinawanyima uhuru waandishi wa habari kufanya kazi zao.

“Mahakama imesikiliza shauri kwa masuala ya awali ambayo ni kukubaliana katika kuwaleta pamoja walalamikaji na walalamikiwa wakubaliane shughuli na mambo yanayolalamikiwa ni yapi, hii ni hatua muhimu kwetu itaamua kesi ikoje na kesi ni ipi.”

Mawakili wanaowakilisha walalamikaji katika shauri hilo ni Wakili Jenerali Ulimwengu, Wakili Fulgence Massawi na Jebra Kambole.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles