31.2 C
Dar es Salaam
Friday, October 11, 2024

Contact us: [email protected]

POLISI: MWANAFUNZI CHUO KIKUU HAKUTEKWA, ALIKWENDA KWA MPENZI WAKE

Na Jones Njozi, Dar es Salaam

Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, limesema mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), na Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi (TSNP), Abdul Nondo hakutekwa ila alikwenda kwa mpenzi wake mkoani Iringa.

Aidha, Jeshi hilo limesema linakamilisha taratibu za kisheria kumsikisha mwanafunzi huyo mahakamani kwa kudanganya na kuzua taharuki katika jamii.

Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amesema leo Jumanne Machi 13, upelelezi imebaini kuwa mwanafunzi huo alikwenda Iringa kwa mpenzi wake ambaye alikuwa akifanya naye mawasiliano mara kwa mara akiwa njiani kuelekea huko katika muda aliosema ametekwa ambapo hadi sasa simu yake imeendelea kuonyesha mawasiliano kati yake na huyo mpenzi wake huyo aliyekuwa anamfuata.

“Machi 6, mwaka huu zilizagaa taarifa katika mitandao ya kijamii kuhusu mwanafunzi huyu kwamba ametekwa, hali iliyozua taharuki kwa wanafunzi wa UDSM, wanafunzi wengine na jamii kwa ujumla.

“Jeshi la Polisi baada ya kupata taarifa hii ilianza ufuatiliaji na kuatika kufuatilia tulilenga kubaini ukweli ambalo tayari lilikuwa limetolewa taarifa mitandaoni na tulifungua kesi yenye kumbukumbu ili kuchunguza na kubaini ukweli wa taarifa hiyo.

“Machi 7, mwaka huu Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam ililetewa taarifa kutoka Jeshi la Polisi Mkoa wa Iringa, kwamba mwananfunzi huyo anayedaiwa kutekwa alipatikana mkoani humo Wilaya ya Mafinga akiwa na afya njema na mwenye kujitambua akiendelea na shughuli zake na wala hakuripoti tukio lolote klabla ya kukamatwa.

“Tuligundua mwanafunzi huyi hakutekwa bali alikjiteka au kuamua kutoa taarifa hizo ambazo kimzingi zilikuwa na maslahi kwake binafs, na pengine kwa kuwa wanasema ni mwenyekiti wa mtandao wa wanafunzi wanaojihusisha na mambo ya siasa pengine alitaka kulizua hilo kwa jili ya kujipatia umaarufu,” amesema Mambosasa.

- Advertisement -

Related Articles

1 COMMENT

  1. nchi yetu imefika mahali pabaya maana hali ya sasa haieleweki kiasi ninaona wasisi wetu hawajacha nchi ikiwa na sura hiikwakweli tunatakiwa tujitafakari ili tusiendelee kupotea

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles