23.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Kerr hawazi chochote ni Azam

dylanker-haiphongKOCHA Mkuu wa klabu ya Simba, Dylan Kerr, amesema kuwa kwa sasa akili yake ameielekeza kwenye mchezo wao dhidi ya Azam FC unaotarajiwa kuchezwa Desemba 12, mwaka huu, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Kabla ya kusimama kwa ligi kuu, Kerr alishuhudia dakika 90 za mchezo kati ya Azam na Toto Africa katika Uwanja wa Chamazi, ambapo vinara hao wa ligi kuu waliibuka na ushindi wa mabao 5-0.

Katika mchezo huo, Kerr aliisifia Azam, akidai kuwa kwa mchezo wanaouonyesha wanastahili kuwa katika nafasi ya kwanza wanayoishikilia kwenye ligi, huku akitamba kuanza kuwafungia kazi rasmi baada ya kurudi mapumziko ambapo tayari ameishaanza kuwapa wachezaji wake mazoezi ya nguvu ili kuwaweka fiti.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Kerr alisema, anautazama kwa umakini mkubwa mchezo huo, kwani anahitaji kujipanga kwa kila namna, ili kuweza kuwakabili vilivyo na hata kuibuka na ushindi.

“Naijua Azam na nimeisoma vizuri, nahitaji kujipanga kuikabili, nauangalia mbali zaidi mchezo huo lakini nahitaji kushinda, nimekuwa akijitahidi kuwapa mazoezi tofauti wachezaji na kuangalia kila idara ili kuhakikisha wanakuwa fiti na hata kuweza kutimiza malengo yao ya kupata ushindi kwa kila mchezo kwa kuanzia na mchezo huo,” alisema.

 

 

 

 

 

 

 

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles