Nairobi, Kenya
Nchi ya Kenya inatarajiwa kupokea Dozi 72,000 za chanjo ya virusi vya Ugonjwa wa Covid 19 kutoka kituo cha covax wiki hii.
Chanjo hizo zilisambazwa kutoka Sudan Kusini baada ya maafisa wa afya wa nchi hiyo kusema hawawezi kuzitumia kabla ya muda wake wa matumizi kumalizika.
Sudan Kusini ilipokea dozi 132,000 za chanjo ya Astra Zeneca kupitia mpango wa Covax mwishoni mwa mwezi Machi.
Waziri wa Afya wa nchi hiyo Mayen Machout alisema hawawezi kutumia chanjo hizo zote kwasababu bunge ilichukua muda kuidhinisha matumizi yake.
Sudan Kusini itasalia na dozi 52,000 ambazo zinatarajiwa kutumiwa kabla ya tarehe 18 mwezi Julai, ambao ndio muda wake wa mwisho wa matumizi.
Mwezi Aprili, Sudan kusini ilisema ina mpango wa kutupa dozi 60,000 za chanjo ambazo muda wake wa matumizi umemalizika walizopokea kupitia msaada wa Muungano wa Afrika.