NAIROBI,Kenya
WANASAYANSI wa Taasisi ya Utafiti wa Afya nchini hapa (KEMRI) wamesema kwamba wamefanikiwa kupata  dawa mpya ya kuzuia Malaria kwa wanawake waja wazito.
Kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa jana mjini hapa, dawa hiyo,ambayo lugha ya kitaalam inaitwa, Dihydroartemisinin-piperaquine (DP), imefanyiwa majaribio katika maeneo mbali nchini likiwamo la  Ahero ambalo lipo Magharibi  mwa nchi na imeonesha kuwa na mafaniki.
Katika utafiti huo, ripoti hiyo inaeleza kuwa dawa hiyo inaonekana kuwa ni salama, na imegunduliwa kuwa salama kwa matumizi ya kuzuia Malaria kwa wanawake wenye ujauzito wa kuanzia miezi minne hadi tisa.
Taarifa hiyo inaweza kuwa habari njema kwa hakina mama wajawazito kutokana na kuwa Ugonjwa wa Malaria una hatari kubwa zaidi kwa  waja wazito.
Kwa mujibu wa Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa (WHO), ugonjwa wa malaria unaendelea kusababisha vifo vya watu kadhaa wengi duniani.
Kwa mujibu wa WHO mwaka 2016, watu  zaidi ya 445 000 walifariki kutokana na Malaria duniani ikilinganishwa na 446 000 waliopoteza maisha  2015.
Watoto walio na chini ya umri wa miaka 5 ndio walio katika hatari zaidi ya kukabiliwa na Malaria
Kwa sasa  WHO inapendekeza dawa ya Fansidar kuwa na uwezo wa kuzuia  malaria miongoni mwa wanawake waja wazito, lakini hata hivyo imekuwa ikishuhudiwa ikishindwa kupambana na makali ya ugonjwa huo na wakati mwingine ikishindwakufanya kazi kwa baadhi ya watu.