25.2 C
Dar es Salaam
Monday, April 22, 2024

Contact us: [email protected]

Kaymu yazindua kampeni ya kusafirisha mizigo bure

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
KAMPUNI ya Kaymu Tanzania, imezindua kampeni ya msimu wa likizo kuwapatia wateja ofa maalumu ya bure ya kusafirishaji mizigo ndani ya Jiji la Dar es Salaam, ikiambatana na bidhaa mpya zenye ubora.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa Kaymu Tanzania, Erfaan Mojgani, alisema lengo la kampeni hiyo ni kusaidia katika ununuzi wa msimu wa likizo na kuwahamasisha watu kutumia fursa ya biashara kwa njia ya mtandao inayokua kwa kasi Afrika.
“Tunajivunia sana kutoa ofa ya bei nzuri kwa bidhaa mbalimbali ambazo tuna imani wateja watavutiwa nazo kwa kipindi hiki cha msimu wa sikukuu.
“Katika sehemu nyingi za dunia, msimu huu ni msimu ambao wauzaji wanakuwa bize zaidi ndani ya mwaka pia kwa Tanzania ndivyo ilivyo, Kaymu inatumaini mwaka huu wanunuaji watagundua kwamba wana njia mbadala mbali na njia ya kwenda kusongamana kwenye masoko mbalimbali na kusimama kwenye mistari mirefu,” alisema.
Alisema kampeni hiyo itaendeshwa kwa muda wa wiki mbili kuanzia Desemba mosi hadi Desemba 14 na oda zitakazofanywa baada ya hapo hazitaweza kufikishwa kutokana na kuongezeka kwa idadi ya oda.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles