33.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, November 27, 2024

Contact us: [email protected]

KATIBU MKUU, MKURUGENZI WASAKWA YANGA

NA WINFRIDA MTOI-DAR ES SALAAM

KLABU ya Yanga imetangaza nafasi mbalimbali za kazi katika klabu hiyo, zikiwamo za katibu mkuu na mkurugenzi wa mashindano.

Tangu kuvurugika kwa uongozi katika klabu hiyo kwa viongozi wa juu kujiuzuru, nafasi ya Katibu mkuu ilikuwa inakaimiwa na Omar Kaya, baada ya Charles Mkwasa kuachia ngazi.

Katika tangazo  la ajira lililotolewa jana na klabu hiyo, nafasi nyingine za kazi zilizotangazwa ni mkurugenzi wa benchi la ufundi na mkurugenzi  wa fedha  na utawala.

Ajira nyingine ni mkurugenzi wa  makoso, mauzo na matukio, mkurugenzi wa sheria na uwanachama, pamoja na tenda ya usambazaji wa bidhaa za  klabu hiyo.

Kati ya sifa zinazohitajika  kwa waombaji wa nafasi hizo ni pamoja na  elimu ya kuanzia shahada ya kwanza, pamoja na uozoefu katika sekta ya michezo na kazi anayohitaji.

Katika nafasi ya katibu mkuu, anahitajika mtu mwenye uelewa wa  mchezo wa soka  kitaifa na kimataifa, pamoja na uozoefu usiopungua miaka  saba na kuhudhuria kozi za  utawala zilizotolewa na Shirikisho La Soka La Kimataifa(FIFA).

Uongozi  mpya wa klabu hiyo chini mwenyekiti Mshindo Msola na Msaidizi wake, Frederick Mwakalebela, umekuwa ukianika mikakati mbalimbali yenye lengo la kuirejesha katika chati, baada ya kushindwa kutwaa ubingwa wa  Ligi Kuu Tanzania bara kwa msimu miwili mfululizo.

Wakati uongozi huo mpya ukizidi kujidhatiti, juzi Shirikisho la Soka  Afrika(Caf)lilithibitisha Tanzania kuwalikishwa na timu nne katika michuano ijayo ya  Ligi ya Mabingwa Afrika na Kombe la Shirikisho.

Kwa mujibu wa kanuni za Ligi Kuu Tanzania  Bara, zilizofanyiwa marekebisho, Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Soka Tanzania( TFF), baada ya kupatikana nafasi nne, timu za Tanzania zitakazowakilisha kwenye mashindano hayo ni  Simba, Yanga, ambazo zitashiriki Ligi ya Mabingwa, wakati KMC  na Azam FC zitashiriki Kombe la Shirikisho.

KMC itaiwakilisha Tanzania Kombe la Shirikisho, kwa mujibu wa kanuni hiyo ambayo inatamka, kama timu iliyomaliza nafasi ta tatu itakuwa ndio bingwa wa Kombe la TFF, basi mshindi wanne  atapata nafasi ya kucheza Kombe la Shirikisho.

Kwa mujibu wa kanuni hizo, bingwa wa Kombe la TFF, ambaye kwa msimu huu ni Azam atawakilisha nchi katika michuano ya Kombe la Shirikisho.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles