32.2 C
Dar es Salaam
Saturday, November 16, 2024

Contact us: [email protected]

Katibu Mkuu CCK mbaronikwa tuhuma za rushwa

Na CHRISTINA GAULUHANGA – DAR ES SALAAM

KATIBU Mkuu wa Chama cha Siasa Cha Kijamii (CCK), Renatus Muabhi anashikiliwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) Mkoa wa Ilala kwa tuhuma za kuomba na kupokea rushwa ya Sh milioni 50, akijifanya ni mtumishi wa taasisi hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Ilala, Christopher Myava alisema Desemba 10,mwaka huu eneo la Vingunguti katika Ofisi za Barry’s Engineering and Contracting Company Limited (BECCO), mtuhumiwa alijifanya mtumishi wa Takukuru na kumuahidi Mkurugenzi wa BECCO, Manraj Bharya ampe Sh milioni 50 ili amsaidie tuhuma alizokuwa anakabiliana nazo za Kampuni ya Kufua umeme (IPTL).

Alisema mtuhumiwa alikamatwa siku hiyo, baada ya kuwekewa mtego wa Sh milioni moja alizozipokea akijifanya atasaidia kumaliza tatizo hilo.

“Baada ya kupata taarifa, tuliamua kuweka mtego na kufanikiwa kumnasa mtuhumiwa akiwa amepokea kiasi hicho,”alisema Myava.

Alisema uchunguzi unaendelea na mtuhumiwa atafikishwa mahakamani wakati wowote.

Kutokana na hali hiyo, alitoa kwa wananchi kutoa taarifa polisi pindi wanapobaini vitendo vya rushwa au ukiukwaji wa haki za msingi kwa lengo la kushinikiza rushwa.

Alisema miezi sita ya mwanzo wa mwaka huu, walipokea malalamiko  yanayohusu rushwa 180, yasiyohusu rushwa 62, majalada yaliyofunguliwa kutokana na malalamiko mapya 42 na yasiyohamishiwa idara zingine hakuna.

Pia yaliyopokelewa malalamiko ya kisekta kwa mwaka wa fedha Januari, mwaka huu  hadi Juni, mwaka huu, ni polisi (31), elimu (7),afya (8), ardhi (15), mahakama (18), Serikali za mitaa (40) na mengineyo 40.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles