22.2 C
Dar es Salaam
Saturday, August 20, 2022

Mufti Zuberi asema msikitiBakwata kukamilika mwakani

Na FERDNANDA MBAMILA-DAR ES SALAAM

MUFTI Mkuu wa Tanzania, Sheikh Abubakar Zuber amesema mradi wa ujenzi  wa msikiti wa Baraza la Waislam Tanzanka (Bakwata), unaoendelea kujengwa Kinondoni,i Dar es Salaam unatarajia kukamilika Februari, mwakani.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana , Zuberi alisema kukamilika msikiti huo, kutasaidia waamini zaidi ya 5,000 kunufaika na jengo hilo.

Alisema pia baada ya kukamilika jengo hilo, litakuwa na maeneo ya biashara ambayo yatasaidia kuongeza pato la baraza hilo.

Alisema tangu kuanza kujengwa kwa msikiti huo wananchi mbalimbali wamejitokeza kudhamini jengi hilo na kuwashukuru kwa msaada wa hali na mali waliyoitoa.

Aliwataja baadhi ya wafadhili hao, kuwa ni  ubalozi wa Morroco, Omani na  Imamarati.

“Lengo la kujengwa kwa msikiti huu, ni kukua kwa taasisi ,kusimamia wafanyakazi kuswalia na kubuni miradi ambayo itaendeleza taasisi hiyo,”alisema Zuberi.

Alisema atahakikisha msikiti huo, unakuwa wa aina yake na wa kimataifa ambapo gharama za ujenzi wake hakutaka kuziweka wazi.

” Tunashukuru wenzetu walioona umuhimu wa kuwapo kwa jengo hili na kutoa msaada kwa ajili ya  mambo mbalimbali na sio kuswalia tu,”alisema.

Alisema ndani ya msikiti huo kutakua na ukumbi wa semina za kidini, mikutano mbalimbali, maduka makubwa ya vyakula  na ukumbi wa mikutano na harusi pia.

“Msikiti huu, utakuwa ni mfano wa kuigwa   kwa Afrika Mashariki nzima,vifaa vyake vilivyotumika vimetoka nchi mbalimbali za kiarabu,”alisema.

Alisema msikiti huo, utapewa jina la Mfalme Muhamad wa 6 kama jitihada za kumuenzi na kukumbuka mchango wake katika dini.

Alisema hadi sasa umekamilika ujenzi wake kwa asilimia 85.

Alisema utakapokamilika watu wa makundi mbalimbali, wanaalikwa kuja kufanya mikutano yao  kwa kupitia ruhusa ya viongozi wa kidini.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
199,057FollowersFollow
551,000SubscribersSubscribe

Latest Articles