24.1 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Kasi ya kipindupindu yazidi kuongezeka Dodoma

????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????NA DEBORA SANJA,DODOMA

KASI ya ugonjwa wa kipindipindu katika Manispaa ya Dodoma inazidi kuongezeka huku kwa sasa kuna wastani wa wagonjwa wapya wanane kila siku.

Kauli hiyo ilitolewa jana na Mganga Mkuu wa Manispaa ya Dodoma, James Charles wakati akizungumza katika kikao cha Kamati ya Afya ya Msingi kilichokuwa na lengo la kuweka mikakati ya kutokomeza ugonjwa huo.

Alisema hali hiyo ya wagonjwa wapya ikiendelea hivyo, Kambi Maalumu iliyotengwa kwa ajili ya kutibu wagonjwa hao itaelemewa kwa ukosefu wa dawa, vifaa tiba, vyakula na rasilimali watu.

“Hadi sasa (jana) wagonjwa waliolazwa walikuwa 48, kama wiki mbili zijazo hali itaendelea kuwa hivi tutakuwa tunapokea wagonjwa wapya 30 kila siku, ikifikia hali hii tutahitaji takribani Sh. milioni 98.7 kwa ajili ya kugharamia matibabu na huduma nyingine,” alisema.
Alisema kwa sasa Tarafa zote nne za Manispaa ya Dodoma tayari zimeshaathirika na ugonjwa huo na kuwataka wadau mbalimbali kushirikiana kuhimiza usafi na kanuni za afya ili kujikinga na maambukizi mapya.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini, Dk. Jasmine Tisekwa, alisema hali ya ugonjwa huo ni mbaya huku akitaka jitihada za haraka kuchukuliwa kuutokomeza.

“Kuanzia sasa hakuna kupika pombe za kienyeji, hakuna kuuza vyakula barabarani ovyo, mama ntilie waache kupika vyakula vyao na marufuku kuwepo kwa mikusanyiko kama vile minada,” alisema.

Aliwataka wadau mbalimbali kushirikiana katika kutokomeza kipindupundu wakiwemo wafanya biashara, Mkurugenzi wa Manispaa ya Dodoma, Shirika la Umeme (TANESCO) Dodoma,Jeshi la Polisi , taasisi mbambali na mabwana na mabibi afya.

“Nawataka pia Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira (DUWASA) muweke dawa ya kuua vimelea kwenye maji yenu kabla ya kuyasafirisha maana hadi sasa hatujajua chanzo cha ugonjwa huo ni nini,” alisema Dk. Tisekwa
Alisema hadi jana wagonjwa 54 wameshaugua kipindupindu na kati yao watano wamepoteza maisha.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles