28.2 C
Dar es Salaam
Friday, November 15, 2024

Contact us: [email protected]

Karia, Kaburu waongoza mazishi ya Asha Muhaji

Zainab Iddy – Dar es Salaam

RAIS wa Shirikisho la Soka Tanzania TFF, Wallace Karia pamoja na viongozi mbalimbali wa soka jana waliungana kumuaga aliyekua Mwandishi mwandamizi na msemaji wa zamani wa Simba Asha Muhaji.

Asha Muhaji alifikwa na umauti siku ya Jumatano baada ya kuugua kwa muda mfupi na kulazwa katika hospitali ya Hindu Mandal, jijini Dar es Salaam.

Enzi za uhai wake, Asha alifanya kazi katika kampuni ya New Habari Ltd, inayochapisha magazeti ya Bingwa, Dimba, Mtanzania na Rai  akiwa mmoja wa waandishi  na wahariri waliofanya kazi kwa weledi mkubwa.

Akizungumza wakati wa kumuaga mwili wa marehemu jana nyumbani kwao  Kijitonyama -Mabatini, Karia alisema Asha alikua mtu makini katika kazi yake, huku akiwa na mchango mkubwa katika maendeleo ya soka la Tanzania kwa ujumla.

“Ni mwanamke aliyepambania kazi yake na kuipenda kutoka moyoni, ndiye mwanamke wa kwanza kuaminiwa na klabu kubwa na kupewa dhamana ya kuisemea timu, nadhani mchango wake umeonekana kwa kila mmoja wetu, kikubwa tumuombee  apumzike kwa amani huko aendako ,”alisema Karia.

Mbali ya Karia pia, Makamu mwenyekiti wa zamani wa klabu ya Simba, Godfrey Nyange ‘Kaburu’, alikiri kuwa Asha amekua na mchango mkubwa ndani ya klabu ya Simba na ndiye mwanamke aliyechangia kuifikisha Simba hapa ilipo sasa.

Mbali na viongozi hao pia alikuwepo Katibu mkuu wa Shirikisho hilo, Wilfred Kidau, Msemaji wa Simba, Haji Manara, Almas Kasongo (Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi) na wasanii mbalimbali.

Mwili wa Asha Muhaji uliswaliwa katika msikiti wa Mwinyimkuu na kisha kuhifadhiwa jana katika makaburi ya MwinyiMkuu yaliyopo Magomeni, Dar es salaam.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles