28.7 C
Dar es Salaam
Sunday, November 28, 2021

Kisa GSM, wanachama wauvaa uongozi Yanga

Zainab Iddy – Dar es Salaam

VIONGOZI wa Matawi  wanachama wa Yanga  mkoa wa Dar es Salaam wameutaka uongozi wa klabu hiyo  kuendelea kufanya kazi na wadhamini wao kampuni ya GSM vinginevyo wajiuluzu .

Kauli hiyo imetolewa jana katika kikao cha  viongozi wa  matawi mkoa wa Dar es Salaam, waliokutana katika Makao makuu ya klabu hiyo yaliopo  Karikaoo Mtaa wa Jangwani.

Kikao hiko cha dharura kimekaliwa kutokana na hivi karibuni kusambaa barua ya GSM kwenda kwa uongozi wa Yanga ikielezea nia ya kampuni hiyo kujitoa kusaidia mambo yaliyopo nje ya mkataba walioingia na Wanajangwani hao.

Akizungumza jana , Mratibu wa Matawi ya Yanga mkoa wa Dar es Salaam, Kaisi Edward , alisema kuwa GSM wamekuwa msaada mkubwa ndani ya timu yao kiasi ya kuwafanya kutembea kifua mbele dhidi ya watani zao hata kama wanapata matokeo ya kuumiza.

“Tangu kuja kwa GSM  ndani ya Yanga, kumeaanza kuonekana taswira ya timu hivi sasa kwa sababu wachezaji wanalipwa kwa wakati, wanakaa katika kambi nzuri na hata kucheza soka la kueleweka ingawa muda mwingine tunapoteza  kutokana na sababu za nje ya uwanja.

“Lakini kuna watu wachache ambao wameamua kutuvuruga kwa kupandikiza chuki kwa viongozi waliopo katika kamati ya utendaji eti wakihoji uhalali wa GSM kufanya kazi  za usajili ambazo zilipaswa kutekelezwa na kamati ya Utendaji kitu ambacho hakina maana kabisa,”alisema.

Kaisi aliongeza: “ GSM ndiye ni sawa na wanachama wengine anatoa fedha kwa mapenzi yake kufanya usajili na kuwalipa wachezaji kwa  faida ya Yanga, lakini leo watu wanaona anaingilia majukumu yao.

“Mwenyekiti Mshindo Msolla na wenzako kama  hamtaki kufanya kazi na GSM ni bora mkajiuzulu kuliko kumuondoa wakati mkijua hamna uwezo wa kutimiza mahitaji yote ya timu na kama mtafanya hivyo    tutatumia nguvu kuwaondoa.”

MTANZANIA lililokuwepo wakati wa mkutano huo, lilimfuata Katibu Mkuu, David Ruhago, katika ofisi yake ili kulizungumzia hilo kwanza alisema hakuna na taarifa na kikao kilichofanywa na viongozi hao wa matawi eneo hilo, lakini kwa sababu ni sehemu ya wana Yanga wote hakuna tatizo.

Kuhusu suala la Yanga na GSM , Luhago alisema: “ Mashabiki, Wanachama na yoyote mwenye mapenzi mema na Yanga asiwe na wasiwasi , tangu  jana  na leo pia kuna vikao  cha kamati ya Uendaji tunakaa  kati yetu na GSM lengo ni kuliweka hili lililojitokeza pamoja na kuangalia namna gani ya kumpa nafasi kufanya yale anayoona ni sahihi kuifanyia Yanga.

“ Hadi kufikia kesho (leo) tutakuwa tumeshaliweka sawa hili , wanachama watulie bado tutafanya kazi na GSM kwa ukaribu na hao wanaowadai ni mamluki tutawachukulia hatu baada ya kubaini yanayozungumzwa yanaukweli,”alisema Kaisi.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
167,206FollowersFollow
526,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles