26.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

‘Afro East’ ya Harmonize yarejea mtandaoni

Christopher Msekena

ALBAMU ya msanii wa Bongo Fleva, Rajab Kahali a.k.a Harmonize, Afro East, imerejea tena mtandaoni baada ya kutoweka kwa ishu zinazohusiana na haki miliki.

Afro East, iliyozinduliwa Machi 14, mwaka huu, ilifanikiwa kufanya vizuri katika mitandao ya kuuza, kusikiliza na kupakua muziki duniani lakini juzi ikatoweka ghafla jambo lililozua taharuki miongoni mwa mashabiki zake.

Akizungumzia kupotea kwa albamu hiyo, Harmonize alisema: “Niwaombe samahani mashabiki zangu wote kwa albamu yetu, Afro East kupotea kwenye ‘platform’ zote lakini Mungu ni mwema tayari imerudi kwenye mitandao ya Apple Music, Spotify, Tidal, Audiomack, Boomplay Music na YouTube.”

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles