25.8 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 26, 2024

Contact us: [email protected]

KARIA AKALIA KITI CHA MALINZI TFF, MADADI ACHUKUA CHA MWESIGWA

Wallace Karia

Na MOHAMED KASSARA-DAR ES SALAAM

KAMATI ya Utendaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), limewakabidhi rasmi madaraka Wallace Karia na  Salum Madadi kulisimamia Shirikisho hilo hadi pale Rais Jamal Malinzi na Katibu MKuu wake, Mwesigwa Celestine  watakapomaliza kujibu mashtaka mbalimbali  yanayowakabili.

Juni 27, mwaka huu Malinzi na Katibu wake, Mwesigwa Celestine  walisomewa mashtaka 28, ikiwamo kutakatisha fedha na kughushi, huku wakiwekwa  ndani hadi Julai 3, mwaka huu.

Kabla ya kukaimishwa nafasi hizo, Karia alikuwa Makamu wa Rais ambaye alishinda nafasi hiyo katika uchaguzi wa TFF uliofanyika mwaka 2013 , wakati Madadi alikuwa  Mkurugenzi wa Ufundi wa Shirikiksho hilo.

Licha ya Karia kukaimu nafasi hiyo, kiongozi huyo ni miongoni mwa watu waliojitokeza kugombea  nafasi ya urais wa Shirikisho hilo katika Uchaguzi Mkuu wa TFF unaotarajiwa kufanyika Agosti 12, mwaka huu mkoani Dodoma.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Madadi alisema maazimio hayo yamefanyika katika kikao cha dharura cha Kamati ya Utendaji na wamefanya hivyo kwa mujibu wa katiba ya TFF,  kifungu cha 35(1) pamoja 36 vilivyotumika kuwakabidhi wadhifa huo.

“Nafasi hizi zitadumu hadi pale kesi itakapokwisha kabisa na viongozi hao watakapokuwa huru ndipo wataendelea na shughuli zao kama kawaida.

“Maazimio haya yamefanyika kuokoa utendaji kazi wa Shirikisho, kwani kuna mambo mengi yamesimama mara baada ya tukio hili ikiwamo suala la Uchaguzi Mkuu pamoja  na uangalizi wa kikosi cha timu ya Taifa kilichopo katika mashindano ya Cosafa,” alisema.

Alisema kwa upande wake nafasi hii ni kubwa na yenye majukumu mengi, kwani yeye amezoea kazi yake kama mkurugenzi wa ufundi lakini hakuna jinsi atakabiliana na changamoto zinazomkabili.

Wakati huo huo, Kamati ya Uchaguzi ya Chama cha Mpira wa Miguu kwa Wanawake (TWFA) imetangaza majina ya wagombea 11 waliopitishwa kuwania nafasi mbalimbali katika uchaguzi mkuu wa chama hicho utakaofanyika Julai 8, mwaka huu mkoani Morogoro.

Majina ambayo yamepitishwa ni Amina Karuma, Rose Kisiwa, Somoe Ng’itu, Theresia Mung’ong’o, Hilda Masanche, Salma Wajeso, Zena Chande, Triphonia Temba, Mwamvita Kiyogoma, Jasmin Soudy na Chichi Mwidege.

Nafasi zinazogombewa ni Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti, Katibu Mkuu, Katibu Msaidizi, Mweka Hazina, Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa TFF na Wajumbe wanne wa Kamati ya Utendaji.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles