28.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Kapteni Semunyu, askari JWTZ wapongezwa mafanikio mchezo wa gofu

Na WINFRIDA MTOI, Mtanzania Digital

KITENDO cha  Klabu ya Gofu ya Lugalo kuendelea  kuwa juu katika mchezo huo,Mnadhimu Mkuu  wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania(JWTZ) Luteni Jenerali Mathew Mkingule, amempongeza Ofisa Habari wa klabu hiyo. Kapteni Seleman Semunyu na askari  wengine wanaocheza gofu kwa mafanikio  waliyopata katika kulitangaza Jeshi  michezoni.

Luteni Jenerali Mkingule  alizungumza hayo jana usiku wakati wa hafla ya ufungaji  na mashindano ya  gofu ya Kombe la Mkuu wa Majeshi ‘CDF Trophy’ ambapo baadhi ya askari waliibuka washindi.

 Amesema  Jeshi  linatambua uwezo wa Kapteni Semunyu, ndiyo sababu likampa majuku hayo na  ubora wameuona katika  majukumu yake ya kuitangaza JWTZ na nchi kwa ujumla  kupitia vyombo vya habari.

“Nimpongeze Kapteni Semunyu, hamjui umahiri wake ulianza kuonekana akiendesha kipindi cha  dakika 45 ITV na sasa tunajivunia kuwa na mtu wa aina yake,” amesema Luteni Jenerali Mkingule.

Mmoja wa washiriki wa mashindano ya CDF Trophy akiwa uwanjani

Ameongeza kuwa kutokana na jitihada za kulitangaza jeshi na nchi hasa katika michezo atafikisha kwa Mkuu wa Majeshi taarifa ya  kazi nzuri inayofanywa na  wachezaji wa gofu askari walioshinda kwenye mashindano hayo.

“Askari mlioshinda mmefanya kazi kubwa ya kuletea sifa JWTZ na Taifa kwa ujumla hakuna budi kupongezwa sambamba na Mwenyekiti kwa kuwalea vizuri kimchezo mpaka kufikia hapo,” amesema.

Aidha amesema  JWTZ ipo katika mpango wa kuhakikisha inajenga viwanja vya gofu  katika mikoa  mingine vile Arusha na Mafinga, Iringa.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Klabu ya Gofu ya Lugalo Brigedia Jenerali Mstaafu Michael Luwongo, ameomba Jeshi kukamilisha ahadi ya Ujenzi wa Uwanja Jijini Dodoma.

Amesema  klabu imejiandaa kutengeneza wataalamu watakaofundiaha mchezo huo mahali popote  watakapohitajika.

Katika michuano hiyo iliyofanyika kwa siku tatu, yakishirikisha wachezaji wa kulipwa na ridhaa, mshindi wa jumla wa  alikuwa  ni Victor  Joseph kutoka klabu ya Dar es Salaam Gymkhana.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles